WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Saturday, December 24, 2011

CHRISTMASS GIFT: OPEN HERE

I wanna take this opportunity as the owner of this Blog/Page to wish all of my fans and friends who visit here every now & then a
MERRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012.
May GOD bless you all and make you to see another 100 Xmass Celebration. Down here its a special message to you in this Christmass eve

"People hurt you
God will heal you
People humiliate you
God will magnify you
People judge you
God will justify you"

From
Ronald Richard Makawa

Monday, December 19, 2011

MVUA YAZUA BALAA DAR ES SALAAM

Mvua iinayoendelea kunyesha ndani na nje ya jiji toka mishale ya saa kumi alfajiri zimezua balaa katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam. Mvua hizo zimesababisha baadhi ya mito jijini hapa kufurika huku mitaro ikishindwa kupitisha maji mengi yanayopita kwa kasi swala ambalo limefanya mitaro hiyo kumwaga maji njiani.
Maeneo ya Ubungo Darajani, Kibangu na Riverside yameonekana kujaa maji ambapo maji yamejaa sehemu nyingi ambapo pia maeneo ya Sinza na Tandale pia hayafai kutokana na kujaa kwa maji. Maeneo ya Manzese na Magomeni hasa eneo la Jangwani pia maji yamejaa na kuzuia barabara katika baadhi ya maeneo.
Sio maeneo hayo tu katika maeneo ya Posta, Gongo la mboto, Mbagala na Kurasini pia yamefurika jambo ambalo limesababisha kuwa na foleni kubwa jijini.
Wakazi wa mabondeni hali ni mbaya mno na juhudi za haraka zinahitajika kuwasaidia watu hawa.

TAARIFA MAALUM TOKA TANESCO

Kutokana na mvua kubwa zinazoambatana na Radi zinazoendelea katika jiji la Dar es salaam toka mishale ya saa 10 alfajiri, zimesababisha kukatika kwa umeme katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nguzo za umeme zimedondoka kama eneo la Ubungo na Tabata Segerea jambo ambalo limeilazimu Tanesco kuzima umeme baadhi ya maeneo kuepusha hatari.
Nikizungumza na moja ya wafanyakazi wa kitengo cha mawasiliano asubuhi hii ambae hakuwa tayari jina lake kuwekwa hapa amesema wananchi wanapaswa kutembea kwa makini wakati huu wa mvua na endapo utaona popote ambapo nguzo imedondoka au nyaya kukatika na matatizo mengine ya umeme toa taarifa Tanesco mara moja, ameendelea kusema katizo hili la umeme ni la muda na hali itakapokuwa shwari watashughulikia baadhi ya maeneo yenye matatizo na shughuli zitaendelea kama kawaida.
Tanesco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Friday, December 16, 2011

RATIBA YA 16 BORA UEFA YATANGAZWA: LOOK DOWN

Ratiba ya mechi za raundi ya 16 bora imetangazwa na UEFA mchana huu na ni kama ifuatavyo

Chelsea vs Napoli
Arsenal Vs AC Milan
Lyon vs Apoel Nicosia
Basel vs Bayern Munchen
Barcelona vs Bayern Leverkusen
Real Madrid vs CSKA Moscow
Inter Milan vs Marseile
Zenit St. Petersburg vs Benfica

Mechi za kwanza zitakuwa kati ta tarehe 14/15

Wednesday, December 14, 2011

BE CARE: WATU 102 WAFA KWA KUNYWA POMBE YENYE SUMU

Watu 102 wamefariki dunia baada ya kunywa pombe inayodhania kuwa na sumu aina ya Methanol katika kijiji cha Sangrampur katika jimbo la Kolkota huko India.
Akizungumzia habari hii, hakimu wa jimbo hilo amesema Narayan Swarup Nigam amesema watu hao walianza kufariki siku ya jumanne na hadi sasa watu wanne wanashikiliwa kwa tukio hilo.
Hii ni tahadhari kubwa kwa wale walevi wa pombe za kienyeji maarufu kama mataputapu ambazo hata muda mwingine tumekuwa hatujui zinatengenezwaje.

Source: BBC

MATUKIO KUMI YAKUKUMBUKWA MWAKA 2011: SOMA HAPA

Ifuatayo ni orodha ya matukio ambayo hayataweza kusahaulika katika mwaka 2011. Matukio haya yamekuwa na rekodi za kipekee jambo ambalo limefanya Blogu yako hii ya kijamii kuamua kuyaainisha tukielekea ukingoni mwa mwaka huu, matukio hayo ni kama ifuatavyo:-
1. BABU WA LOLIONDO (KIKOMBE)
Ni moja ya stori ambazo zilizagaa kila sehemu ndani na nje ya nchi hii, Babu ambae ni mchungaji Ambilikile Mwasipile aliyekuwa akitoa dawa kwa mfumo wa kikombe alifanikiwa kuwapatia zaidi ya watanzania milioni 5 dawa iliyokuwa inaaminika kutibu magonjwa mbalimbali sugu. Nani anaweza kubisha hii haikuwa habari kubwa?

2. AJALI YA FIVE STARS MODERN TAARAB
Ajali ya kundi maarufu la Taarab la Five Star Modern Taarab iliyotokea eneo la Mikumi Mkoani Morogoro, 22 March na kuua wasanii 13 wa kundi hilo ilikuwa moja ya tukio kubwa kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi yetu kwa wanamuziki wengi kiasi hicho kupoteza uhai. Mungu awalaze pema peponi

3. UCHAGUZI WA IGUNGA
Ni tukio jingine la kusikitisha katika mwaka 2011 ambapo tulishuhudia ndugu zetu wengi wakipoteza maisha katika fujo za uchaguzi huo huku pakiwa na matumizi mabaya kabisa ya pesa hasa kwa Chama tawala. Tulishuhudia matukio mengi ya udhalilishaji na uvunjifu wa haki za binadamu jambo ambalo lilichafua sifa ya Taifa hili. Mungu azilaze roho za mashujaa waliofariki wakipigania haki

4. JAIRO SKENDO
Ni miongoni mwa habari zilizopewa kipaumbele mno katika mwaka 2011 ambapo katibu huyu wa wizara ya nishati na madini alizichangisha taasisi 20 zilizochini ya wizara hiyo milioni hamsini kila moja kwa ajili ya kuhonga ili bajeti mbovu ya wizara yao ipitishwe. Swala hilo linaingia kwenye orodha hii kwa kuwa ni jambo jipya masikioni mwetu na ni ufujaji wa pesa za umma huku maamuzi ya kurejeshwa kwake kazini na kuondolewa tena ilikuwa kitendawili pia.

5. MISAADA YENYE MASHARTI YA KUUKUBALI USHOGA
Ni kauli iliyowaacha wengi vinywa wazi toka kwa Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron dhidi ya nchi zilizochini ya Jumuiya ya Madola ambapo alizitaka nchi hizo kuzitambua hali za mashoga na wasagaji katika jamii kama kigezo cha misaada. Aliendelea kwa kudai watakaokiuka wasingepatiwa misaada jambo ambalo lilipingwa ba wengi.

6. KIFO CHA OSAMA BIN LADEN NA MUAMMAR GHADAFI
Hawa ni watu wawili tofauti walioitikisa dunia kwa matukio tofauti, vifo vyao vilizua mjadala mkubwa ambapo wengi hawakuamini juu ya vifo vya miamba hii. Tukianza na Osama Bin Laden ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda aliuawa mwezi wa 5 huko Pakistan na kifo chake kuzua utata mkubwa baada ya mwili wake kutoonyeshwa huku Ghadafi akiuawa mwezi 10 na wapiganaji Wa NATO sambamba na waasi wa nchi hiyo.

7. AJALI YA MELI HUKO NUNGWI
Ni ajali inayofananishwa na ile ya MV Bukoba iliyotokea mwa 1996 ambapo maelfu ya watu walipoteza maisha. Katika ajali hii ya meli ya MV Spice ilishuhudia watu zaidi ya 250 kwa mujibu wa serikali walipoteza maisha kutokana na ajali hiyo ya kizembe.

8. MILIPUKO YA MABOMU GONGO LA MBOTO
Ni miongoni mwa tukio lililotokea mwaka huu na kuanza majonzi makubwa baada ya mabomu yaliyokuwa yamehifadhila katika maghala ya kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto. Watu zaidi ya 500 walijeruhiwa vibaya katika milipuko hiyo, wengine zaidi ya 30 wakipoteza maisha na makazi ya watu zaidi ya 5000 yaliharibiwa.

9. KUJIVUA GAMBA
Ni moja ya kauli ambazo haziwezi kuondoka midomoni mwa watu kirahisi, hii ilikuwa kauli mbiu toka kwa CCM ambapo ilikuwa ikiwataka viongozi wa Chama hicho wenye kashfa kujiuzulu ambapo 14 Jully mbunge wa Igunga Rostam Aziz alijivua gamba huku wengine wakigoma na baadae swala hilo kusitishwa na Rais baada ya Mh. Lowasa kuja juu na kumwaga mboga........ Simo

10. MATUMIZI MAKUBWA KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU NA SWALA LA POSHO
9 dESEMBA mwaka huu ilikuwa ni siku ya kuadhimimisha miaka 50 toka nchi hii kupata uhuru wake, tulishuhudia sherehe kubwa za kuonyesha ufahari huku nchi ikiwa katika orodha ya nchi masikini za kutupwa ambapo tupo katika nafasi ya 152 kati ya nchi 189 zinazoendelea na nchi ya tatu kwa kupatiwa misaada baada ya nchi zenye vita za Iraq na Afghanstan. Katika sherehe hizo fedha zinazokadiriwa kufikia sh 64 bilioni zilitumika. Sina mengi ya kusema juu ya hilo na swala la mwisho ambalo utata wake unaendelea ni posho za wabunge zinazotakiwa kupandishwa na kuwa shilingi laki 3 na 30 kwa kikao ambazo ni shilingi 80 za kujikimu, shilingi 50 za mafuta na posho kwa siku ambayo ni laki mbili.
Mungu ibariki Tanzania

Source: Ronald Richard Library
Tanzania Newspapers
Jamii Forum
Online search Engines

Tuesday, December 13, 2011

5 FACTS ABOUT FACEBOOK USERS IN tANZANIA

Facebook is a social networks that links and create friendship and networking to many people worldwide, but some of illiterate people start to misuse it and label it as a place to show how foolish the're. Below are five facts about Facebook friends in Tanzania.

1. Fake reality is the first fact for friends in Facebook, many of them fake they are names, pics and relationship status, be care with them and take 10% only of people's profiles.

2. Distortion is the second fact, take only few of what they post otherwise you will destroy your mind with foolish & nonsense, how can someone post naked or half naked pics of him/her? And when people ask him/her, he/she end up by saying dats me, be care friend

3. Exploitation of Sex and Manipulation is another fact where some of bums & nuts are here to destroy others reputation and respect infront of others. If your love leaves you here is not a right place to tell us what happen, reality stays there your nothing thats why he/she leaves you. To send his/her naked pics or tell her abusive words is not the solution

4. Murder of character is another fact about facebook friends in Tanzania where some of foolish people open an account for the sake of destroy others reputation bya telling lies and wrong facts about other. Its better if you open an Taarab Band and speak your nonsense there.

5. Illiteracy is the last fact about facebook friends of Tanzania, a lot of people they dont know what to post and at which time, not all the time we are there to Joke and sometimes its important to stay quite instead of writting shits. You must have a claim that is supported by reasons and evidence its how you can write well. Most people in Facebook listen a half, understanding only quarter of what they hear and speak a lot. Be carefull with selection of friends. Its better to have ten real friends than having 500 fake & foolish friends.
Mark my words, if you go somewhere with nine foolish people know that your number ten of them, friends reflects who you are and some of people sees you from your friend.

Friday, December 9, 2011

MISAMIATI 30 ILIKOSA MAJIBU KATIKA MIAKA 50 YA UHURU

Hii ni orodha ya maneno ambayo yamekosa maana ya moja kwa moja na yametesa sana vichwa vya watanzania.
1. Kuchakachua
2. Mchakato
3. Uwekezaji
4. Posho
5. Katiba
6. Maisha bora kwa kila mtanzania
7. Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya
8. Megawati
9.Kujivua Gamba
10. Hadidu za rejea
11. Barabara za juu
12. Mabasi ya mwendo kasi
13. upembuzi yakinifu
14. Sharobaro
15. Fursa sawa kwa wote
16. Richmond
17. EPA
18. Rasimu
19. Kamati teule
20. Tume ya uchunguzi
21. Mfumuko wa bei
22. Muafaka
23. Maslahi ya umma
24. Utandawazi
25. Ruksa
26. Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele
27. Wahisani
28. Kichwa cha mwenda wazimu
29. Haki za Binadamu
30. Mafisadi

Wewe kama mtanzania mwenzangu hebu changia ulichoelewa katika misamiati hii.

Thursday, December 8, 2011

VIBAKA WAMFANYIA KITU MBAYA DIAMOND

Yule mkali wa bongo anaetesa na kibao cha Mawazo kwa sasa baada ya kusumbua na vibao kadhaa kama vile Moyo wangu, Nitarejea na Mbagala, Diamond Platinum a.k.a Baba Wema juzi akitokea kwenye shughuli za kurekodi video yake mpya ya mawazo alipaki gari yake nje ya sehemu anapoishi na alipoingia ndani tu jamaa wenye vyao wakakomba vitu kibao
Akizungumza kwa huzuni, Diamond amesema miongoni mwa vitu vilivyochukuliwa ni pamoja na power window zote, radio, system ya AC na begi lililokuwa na nguo, cheni kibao za gold na saa nyingi alizokuwa akizitumia katika kushoot video yake mpya ya mawazo.
Pole sana mtu mzima

Tuesday, December 6, 2011

HIVI RAIS YUPO AU AMESAFIRI? NCHI INAONGOZWA NA NANI?

Naukumbuka wimbo mmoja wa taarab unaimbwa "Jahazi likikosa nahodha chombo huenda mrama". Haya ndiyo yanayoendelea sasa hapa nchini. Mambo makubwa mengi yanatokea na kiongozi wa nchi yupo kimya tueleweje?
Tanesco wanampango wa kuongeza umeme mara tatu na hatujaona kauli yoyote toka kwa kiongozi wa nchi kama akivyoahidi ataboresha maisha ya wananchi. Posho zimepandishwa na kwa ujumla sasa mbunge atakuwa akipewa 330,000 kwa siku atakapohudhuria kikao kimoja cha bunge kima ambacho ni mshahara wa mwalimu anaeanza kazi.
Hivi kwa mtindo huu tunategemea maandamano yapungue au kuisha? Maisha yapo juu na mfumuko wa bei umekuwa juu sambamba na kushuka kwa thamani ya shilingi, tulitegemea Rais angetoa tamko la jinsi ya kudhibiti haya yote ila imekuwa kinyume kabisa.
Wananchi inapaswa tuamke sasa na tuchukue hatua, hivi palikuwa na haja gani ya kutumia mamilioni yote hayo kusherekea miaka 50 ya Uhuru? Inamnufaisha nini mwananchi wa kawaida? Miaka 50 ya uhuru ni kwa ajili ya viongozi wanaojiongezea mishahara kila wanapojisikia na ingekuwa heri kama wananchi wangezisusia sherehe hizi za kinafki.
Nchi imeshika nafasi ya tatu kwa kupewa misaada duniani na ya kwanza Afrika, nafasi ya juu kwa rushwa na miongoni mwa nchi 50 maskini zaidi duniani. Kwa mtindo huu kazima tulazimishwe kuukubali ushoga ili tupewe misaada. Tafakari, chukua hatua.....

Saturday, December 3, 2011

TUNDAMAN APATA AJALI MBAYA

Msanii maarufu wa kundi la Tiptop Connection maarufu kwa jina la Tundaman au Mikidadi amepata ajali mbaya ya gari akiwa njiani toka Kahama kuelekea Shinyanga kwa ajili ya Shoo.
Tundaman amesema chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na kuchoka kwa dereva ambae alianza kusinzia na kusababisha gari yao aina ya Toyota Cresta kupinduka kichwa chini miguu juu.
Katika safari hiyo Tundaman aliongozana na Dj Kman(wa kundi la Tiptop) na dereva ambae alifariki papo hapo. Hali zao zinaendelea vizuri na mungu awape afya njema

Friday, December 2, 2011

MAKUNDI YA EURO 2012 YATANGAZWA. LOOK DOWN

Makundi ya michuano ya Euro 2012 itakayofanyika huko Poland & Ukraine yametangazwa. Makundi hayo ni kama ifuatavyo
Group A
Poland, Greece, Russia, Czech Republic
Group B
Holland, Denmark, Germany, Portugal
Group C
Spain, Italy, Republic of Ireland, Croatia
Group D
Ukraine, Sweden, France, England
Katka makundi yote kundi B ndilo linaonekana gumu zaidi katika michuano ambao inaonekana itakuwa yakuvutia.

Thursday, December 1, 2011

MR EBBO AFARIKI DUNIA

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipyaAbell Motika maarufu kama Mr Ebbo amefariki dunia huko mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo.
Msanii huyo maarufu ambae enzi za uhai wake alitamba na nyimbo kama Mi mmasai, maneno mbofumbofu, kamongo na mnisamehe huku akighani kwa staili ya kimasai amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi. Msanii huyo pia alikuwa mmiliki wa studio ya Motika Records.
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahala pema peponi.

Wednesday, November 30, 2011

MANCHESTER UNITED WATUPWA NJE:CARLING CUP

Timu kongwe ya Manchester United imetupwa nje ya michuano ya Carling cup na Timu ya dataja la pili ya Crystal Palace kwa magoli 2 - 1.
Mchezo huo yliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford umeshuhudia Crystal Palace wakipata magoli yao kupitia kwa Darren Ambrosse 65' na jingine katika dakika za nyongeza kupitia kwa Glenn Murray 98' ambapo Manchester United walipata goli kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Federico Macheda 69'.
Haya yamekuwa matokeo mabaya zaidi kwa Manchester a,bao wanaonekana kusuasua baada ya sare mbili katikati na mwishoni mwa wiki dhidi ya Benfica katika Klabu Bingwa Ulaya na Newcastle United katika ligi ya Uingereza.

Wednesday, November 23, 2011

BREAKING NEWS; WANNE WAFA KWA AJALI UBUNGO

Watu wanne akiwemo mama mjamzito na wanaume watatu wamefariki papo hapo kutokana na ajali iliyolihusisha Lori la mafuta na Gari ndogo mbili katika eneo la Riverside Ubungo majira ya saa10 jioni. Watu wengine watatu wamewahishwa hospitali kwa matibabu zaidi akiwemo dereva wa moja ya magari hayo madogo na mchuuzi wa barabarani
Lori hilo lililokuwa likielekea bandarini kupitia barabara ya mandela limeangukia magari hayo mawili yaliyokuwa kwenye foleni upande wa pili wa barabara ya kuelekea ubungo mataa katika eneo la Riverside baada ya kujaribu kuikwepa gari nyingine ndogo na kuacha barabara.
Habari zaidi baadae

Tuesday, November 22, 2011

26th Nov; BAADHI YA WASANII WATAKAOTUMBUIZA ; okoa music wa bongo

MR II

G SOLO

ANTI VIRUS PART 1 COVER

SOGGY DOGGY

ZAY B


SUMA G
Picha za juu hapo ni baadhi ya wasanii watakaotumbuiza siku ya tarehe 26 mwezi 11/2011 pale kwenye viwanja vya Sayansi au viwanja vya Posta. Kama mwanaharakati unakaribishwa katika show hiyo kwa kiingilio cha shilingi 5000 tu. Wasanii wengine watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Inspector Haroon, Mkoloni, D wa Gheto, Dani Msimamo, Adili Mkwela, LWP, Coin one, Magazijuto, Peen Lawyer, Mapacha PKP na Rama D. Djs watakaofanya mambo siku hiyo ni Dj JD "John Dilinga" na Majey. pia patakuwa na uzinduzi wa Antivirus Part II, pia unaweza download copy yako kupitia www.swahilioriginaltz.com

Thursday, November 17, 2011

KUNA UMUHIMU GANI KWA KATIBA YETU KUANDIKWA KWA LUGHA YA KIINGEREZA?

Napata wakati mgumu jinsi ya kuandika makala hii, nagundua bado viongozi wetu wengi wana utumwa wa kifikra, hivi ipi ni lugha ya Taifa!!? Kiswahili na Kiingereza? Kwanini tunashindwa kuiheshimu na kuithamini lugha yetu? Hizi ndizo sababu hata shilingi yetu imekuwa ikiporomoka kila siku na gharama za maisha kuzidi kuongezeka sababu wapo viongizi na makampuni ambayo hadi sasa wanalipa au kulipwa kwa dola ndani ya nchi hii, bodi ya TCRA ilikuwa mfano tosha, tuachane na haya
Nashindwa kuelewa kama huo muswada wa katiba unaoleta utata bungeni kama uliandikwa hapa nchini au kwa Cameron!!!
Swali jingine gumu ninalokosa jibu lake kuna nini ndani ya muswada huo wanaokataa kuuweka katika lugha ya Taifa? Mpaka lini tutaendelea kunyenyekea lugha za wenzetu huku tukiongea kinafki kuwa kiswahili ni lugha ya Taifa?
Watanzania wangapi wenye uelewa fasaha wa lugha ya kiingereza? Hata wale wachache waliofanikiwa kupata elimu ya sekondari na elimu ya juu bado lugha hii ni changamoto kwao. Hivi hii katiba wanaandikiwa kina nani? CCM wana ajenda gani ya siri juu ya katiba hii? Siungi mkono wanachofanya CHADEMA kwa sasa bungeni ila ndio njia pekee ya kuonyesha kutoridhishwa na udikteta wa chama tawala.
Wapo baadhi ya wabunge wanapenda kuonekana wema mbele ya Rais na mwenyekiti wao wa chama wamekuwa wakisimama bungeni na kuzungumza upuuzi ambao nawaza bado wananchi wao ndicho walichowatuma? Ufike wakati tuzungumze ukweli na kuacha siasa za kishabiki, hili ndilo tatizo lililofanya wananchi wengi wa kawaida kutoielewa katiba ya zamani hadi sasa.
Patolewe machapisho mengi ya muswada huo wananchi wengi wapate kuelewa nini kinazungumziwa, katiba sio kwa ajili ya chama au wabunge, ni ya wananchi wote. Tuache umbumbumbu wa fikra, mawazo sahihi huja kwa lugha sahihi na inayoeleweka kwa wengi

Wednesday, November 16, 2011

URAIS 2015 WAWACHANGANYA WENGI:TABIRI ZA MASANGOMA ZAPEWA NAFASI KUBWA

Kinyang'anyiro cha Urais wa mwaka 2015 umeendelea kuwapa tumbo joto baadhi ya vigogo wa CCM huku kila mmoja akitumia kila njia kuhakikisha yeye ndie anapitishwa kama mgombea.
Fukuto kubwa linaonekana kwa vigogo watatu wenye nguvu ndani ya Chama hicho ambao wamekuwa wakitumia kila njia kuhakikisha majina yao yanang'ara.
Baadhi ya vigogo hao wamekuwa wakihusishwa na mpasuko mkubwa unaoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi, ambapo baadhi wamekuwa wakiunga mkono wale wanaojihusisha na ufisadi wang'olewe ndani ya Chama, wengine wakipinga hilo na baadhi wakionekana kutounga mkono upande wowote.
Wengine wameenda mbali zaidi na kudai kuwa Rais ajae lazima atoke dini fulani kutokana na mlolongo wa wale waliopita kufuata mapokezano ya dini ambapo imekuwa wanaanza Wakristo na kufuatia Waislam jambo ambalo limewapa nguvu baadhi ya vigogo hao ambao ni wakristo kudhani kuwa sasa ni zamu yao. Huku hayo yakiendelea vyama vya upinzani vimeendelea kujipanga kuhakikisha nao wanachukua madaraka na jambo kubwa ambalo wanafanya sasa ni kuhakikisha wanajijengea sifa nzuri kwa wapiga kura.

HOW TO STOP MASTERBATION ADDICTION

Before you make an attempt to stop masturbating, there’s an important issue to deal with first. This issue is important because masturbation is a misunderstood addiction.

There are people who think they’re addicted to masturbation and they aren’t. Plenty of people are hooked on masturbation and think there’s nothing wrong with it. Just like the alcoholic who fools him or herself about drinking, the person addicted to masturbation is not doing themselves any favor by trying to deny the problem.
Let’s assume you’ve decided that you are addicted to masturbating. There are many people who are addicted to masturbation and hate themselves for masturbating. Feeling let down in yourself for acting addictively is a signal from nature that you are engaging in a pattern of activity that is self-destructive. But feeling let down in yourself is different than self-hatred. When you hate yourself you condemn your total being. When you feel let down in yourself, you are upset with a certain part of your life.

Self-hatred will not help you stop masturbating. One of the things to understand about self-hatred is: You won’t do something good for someone you hate.

People from all walks of life: the devoutly religious, atheists, agnostics, and people who are moderate in their belief system can find themselves smothered in self-hatred because they are addicted to masturbation and can’t stop.

You might be thinking, “If I have a problem hating myself, how do I stop it?” I can tell you where to start: Evaluate yourself the same way you would evaluate someone else who you were trying to be fair to.

For instance, Paul is addicted to masturbation. He wants to stop. He has been trying ever since he was a teen. He can stop for a few days, a few weeks, or even a few months. But eventually he returns to his masturbation addiction. When he returns he descends into self-hatred. Any person who stops addictive behavior and returns to it will feel let down. But Paul is going beyond feeling let down. He hates himself because he can’t stop masturbating.

If you share his problem here’s my advice to you:

“First, give yourself credit for what you accomplished. You wanted to stop. You gave it a best effort. And you succeeded for a while. Would you hate someone else because they attempted to overcome their problem or would you give the person credit for trying?

“If the person failed would you hate him or her? Or would you try to understand that they did their best? If the person has failed many times would you hate him for failing or would you give him credit for continuing to try in face of failure? If the person was concerned about their problem would you hate her because she was concerned or would you give her credit for identifying her problem and wanting to do something about it?”

Remember, you’re not going to be supportive of a person you hate. You will be on the side of someone who’s trying their best.

Some people think that failure at overcoming a masturbation addiction means you don’t want to stop. There’s more to stopping than just wanting to.

  • You need an effective method. “Just say ‘No’” doesn’t work.
  • You need an understanding of addiction. Being addicted and understanding what an addiction is are two very different states of mind.
  • You need to know the differences between a sex addiction and other kinds of addiction. A big mistake people make when they try to deal with a sex addiction is treating a sex addiction as if it were an alcohol problem. A good example of this is the twelve-step approach. Twelve step is an alcohol program. It is not designed and is not effective for sex addiction.
  • You need to know what makes a masturbation addiction different from other kinds of sex addiction. The Most Personal Addiction will give you an in depth discussion of the differences.
  • You also need to determine if you are addicted to masturbation. The interviews in The Most Personal Addiction will help you understand if you have a sex addiction and will help you begin the process of getting a masturbation addiction stopped. There is also a further discussion about masturbation addiction in the article Masturbation Addiction Counseling.

Tuesday, November 15, 2011

MOTO MKUBWA WALIPUKA MITAMBO YA UMEME UBUNGO:MITAMBO YAENDELEA KUTEKETEA NA MOTO

Moto mkubwa umezuka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya ubungo ambayo imepelekea baadhi ya Transformer kuendelea kuungua.
Moti huo ambao chanzo chake hakijafahamika unaendelea kuunguza mitambo hiyo huku pakiwa hakuna jitihada zozote za kuzima moto huo.
Uzembe uliojionyesha dhahiri ni kukuosekana kwa maji kwa gari la zimamoto ambalo hupaki pembezoni mwa mitambo ya Songas.
Hali inaonekana kuwa mbaya zaidi na foleni ni kubwa jambo ambalo litakuwa gumu kwa gari za zimamoto zinazotoka mbali na eneo hili. Idadi kubwa ya wafanyabiashara ambao hupanga bidhaa zao maeneo haya wanakusanya vitu vyao ili kurejea majumbani huku transformer mbili zikiendelea kuteketea
Tega sikio zaidi nipo eneo la tukio

Monday, November 14, 2011

BREAKING NEWS: MAFURIKO DAR NA MWANZA

Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeanza kuleta athari hasa kwa wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni. Mvua hizo zilizoanza kunyesha mapema mwezi huu athari zake zimeonekana zaidi katika jiji la
Dar es salaam na Mwanza ambapo baadhi ya familia zimekosa makazi kutokana na hali hiyo.

Dar es Salaam
Mvua hizo ambazo zimeanza kunyesha mfululizo kwa siku tatu athari zimeonekana zaidi katika maeneo yenye mifumo mibovu ya upitishaji maji taka. Maeneo kama Tandale kwa Mtogole, kwa tumbo, Shoppers & My FAIR Plaza mikocheni yamezungukwa na maji kabisa jambo ambalo limefanya wanunuzi wanaotumia usafiri wa pikipiki na waenda kwa miguu kufika kwa tabu. Maeneo mengine yaliyokubwa na mafuriko hayo ni Manzese, kimara sambamba na daraja la mlalakuwa katika barabara itokayo Magomeni kuelekea Kawe.

Mwanza
Katika jiji la Mwanza pia mvua hizo zimesababisha maeneo kadhaa katika jiji hilo mfano Nyegezi, Majengo Mapya na Nyamagana kufurika maji na kubwa zaidi ikiwa ni kujaa kwa maji kwa Uwanja wa ndege jambo lililofanya ufungwe kwa muda usiojulikana.
Tahadhari inahitajika kabla ya majanga kama haya na tunaombwa kuwapa msaada wale walioathiriwa na mvua hizi. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote inayoyahusisha mafuriko haya na vifo.

Friday, November 11, 2011

NCHINI INANUKA:MNADHIMU MKUU WA JWTZ AKAMATWA NA INTERPOL KWA UFISADI WA TRILIONI 3

Mnadhimu mkuu wa Jeshi la wananchi la Tanzania Abdularahman Shimbo anashikiliwa na polisi wa kimataifa (Interpol) kwa mahojiano zaidi baada ya kuhusishwa na ufisadi wa Shilingi Trilioni 3 ambazo alikuwa amezihifadhi katika benki moja mchini Afrika Kusini.
Chanzo cha habari kinaendelea kupasha kuwa fedha hizo zilitokana na makato ambayo amekuwa akiwakaya wanajeshi wanaoenda kujitolea kulinda amani katika nchi katika nchi mbalimbali na nyingine zikiwa ni shukrani kwa majeshi yetu kwenda kulinda amani katika nchi hizo mojawapo ikiwa Comoro.
Alipofahamishwa swala hilo alizimia na polisi hao wameondoka nae kwenda nchini Afrika Kusini.
Sakata hilo liligundulika baada ya Rais Jakaya Kikwete kwenda nchini Afrika Kusini kuomba msaada na ndipo alipoelezwa wanaombaje msaada wakati kuna mfanyakazi wa kawaida tu wa serikali ana kiasi hicho cha pesa? Ndipo Rais akaagiza uchunguzi ufanyike na baadae swala hilo likagundulika.
Stay tuned kwa habari zaidi

Wednesday, November 9, 2011

FROM MOVENPICK TO DAR ES SALAAM SERENA HOTEL:KWELI HII NCHI WANAIFAIDI WAJANJA

Ule mchezo wa kubadili majina kila baada ya miaka kadhaa ikiwa ni janja ya kukwepa kulipa kodi umeendelea kudhihirika mara baada ya hotel maarufu iliyowahi kuwa na majina zaidi ya kumi katika kipindi kisichopungua miaka 10 kubadili jina, hoteli hiyo ya kisasa iliyokuwa ikifahamika awali kama Sheraton, Royal Palm na baadae Movenpick sasa imepata jina jipya ambalo ni Dar es Salaam Serena Hotel.
Wadadisi wa mambo wanadai janja hii ya kubadili majina inalenga kukwepa kodi ambapo hadi sasa kuna kampuni za simu ambazo pia huu umekuwa mchezo wao ambapo haipiti miaka mitano lazima wabadili jina.
Kwa mtindo huu inamaana serikali imefumba macho? Au watendaji wamepoozwa kidogo? Jibu mimi sina.