WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Saturday, October 29, 2011

MAKALI YA MGAO WA UMEME KUREJEA UPYA: WAZIRI WA FEDHA AGOMA KUTOA FEDHA ZA UNUNUZI WA MAFUTA KWA IPTL

Mgao wa umeme ambao ulisitishwa kwa muda na serikali baada ya kuamua kutoa fedha ajili ya ununuzi wa mafuta kwa kampuni ya IPTL kwa mwezi Agosti na Septemba unaelekea kurejea baada ya Waziri wa Fedha Mh Mustafa Mkullo kugoma kutoa fedha hazina kwa ajili ya zoezi hilo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Mkullo alisema "Sema kabisa kwamba Waziri wa Fedha kasema wizara yake haihusiki na malipo hayo", aliendelea kwa kusema serikali haiwezi kutumia hela za walipa kodi kuyapatia makampuni yaliyoajiriwa na Tanesco ajili ya kuzalisha umeme.
Kampuni ya IPTL inachangia kiasi cha Megawati 80 katika gridi ya Taifa na kama itashindwa kuzalisha kiwango hicho hii inamaanisha makali ya mgao yatarejea kama awali, msemaji wa Tanesco Badra Masoud amesema shirika hilo linatumia zaidi ya bilioni 17 kwa mwezi ajili ya ununuzi wa mafuta kiasi ambacho ni kikubwa mno kwao na kusitishwa huko kwa fedha kutaiingiza nchi kwenye mgao mkali tena.
Aliongeza kuwa kiwango cha maji kwa sasa katika bwawa la Mtera ni kidogo kuzingatia kiwango cha 690mm ambacho ndio sahihi kwa ajili ya kuzalisha nishati hiyo ila wameiombwa Wizara ya maji na wamewakubalia kuanza shughuli hiyo huku akisema hata kukatika kwa umeme mara kwa mara kunatokana na matatizo hayo.
Mgao wa umeme ulipungua makali yake baada ya makampuni ya Symbion 37megawati, IPTL megawati 80 na AGGreko 75megawati kuchangia kiasi cha Megawati 192 katika gridi ya Taifa. Tujiandae ma mgao kwa kweli.
Hii ndio Tanzania

Thursday, October 27, 2011

ZITTO AHAMISHIWA ICU:ANA VIJIDUDU 150 VYA MALARIA, WAJIPANGA KUMPELEKA INDIA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe jana usiku alihamishiwa katika Kitengo Cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum (ICU) baada ya madaktari kutoridhishwa na hali yake.
Msemaji wa Hosipitali ya Muhimbili(MHN) Jeza Waziri amesema madaktari bingwa waliompima Zitto wamegundua kuwa ana vijidudu 150 vya malaria hali ambayo siyo ya kawaida kwa binadamu na ndio sababu iliyofanya madaktari hao kumhamishia katika kitengo hicho.
Wakati huo huo Spika wa Bunge Anne Makinda baada ya kufika hospitalini hapo na kumjulia hali aliwaambia waandishi wa habari kuwa tatizo la kichwa bado linamsumbua Mh Zitto na serikali inajipanga kumpeleka India kwa matibabu zaidi.
Hali ya mheshimiwa Zitto ilianza kuwa tete mapema wiki hii ambapo aliwahishwa katika Hospitali ya Agha Khan na baadae kuhamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi, Mh Zitto alipohojiwa alisema kwa kifupi tu "naendelea vizuri" madaktari wamekataza watu mbalimbali kufika hospitalini hapo kuzungumza na Zitto wakiwamo waandishi wa habari.
Wakati huo huo mbunge wa viti maalum (CUF) Claradiana Mwatuka nae amelazwa katika kitengo hicho kutokana na kusumbuliwa na vidonda vya tumbo, mbunge huyo alifikishwa hospitalini hapo jana na hali yake inaendelea vizuri pia.
Tumwombe mungu awaponye viongozi wetu warudi katika majukumu yao ya kitaifa.

Saturday, October 22, 2011

WATATU WAFA KWA KIPIGO CHA POLISI DODOMA: NANI ANAWAPA HAWA POLISI NGUVU HII?

"Tanzania hakuna amani"x 4 ni kilio kilichoonekana ka,a wimbo nilichokisikia nikiwa nimetegea sikio taarifa ya habari katika stesheni fulani maarufu hapa nchini usiku wa leo, nimepatwa na mshtuko mkubwa ulionifanya nikae chini na kuandaa makala hii. Ni kilio toka kwa wananchi toka Dodoma, makao makuu ya nchi waliokuwa wakipokea kipigo toka kwa askari polisi wakifukuzwa kumpisha mwekezaji katika eneo alilouziwa.
Matukio ya polisi kupiga Raia katika utawala huu wa awamu ya nne yamekuwa ni gumzo lisilomalizika, maeneo ,mbalimbali hapa nchini matukio haya yamekuwa ni wimbo usiomalizika pasina hatua yoyote madhubuti inayochukuliwa na serikali hii dhaifu.
Hebu jiulize hao wawekezaji toka nje wanaouziwa maeneo waliyoyatunza mababu zetu na kuturithisha, na watanzania wazalendo wapi wenye haki? isitoshe wawekezaji wenyewe wanapopewa hayo maeneo huishia kuyatumia kwa manufaa yao huku wananchi wa kandokando inapopatikana miradi hiyo wakiachwa katika hali ngumu. Hakuna shule, hakuna maji na huduma nyingine muhimu, mwekezaji huyu ana faida gani?
Swali kubwa lililobaki kichwani mwangu ni au kwakuwa maeneo yale wanakaa fukara? Mbona kuna viongozi wanamiliki maelfu ya hekari na hatusikii migogoro ya ardhi yao na wawekezaji? Hao polisi waliopiga wananchi huko Dodoma na kuharibu mali zao wanapewa nguvu na nani? Unadhani ni pesa kiasi gani inatosha kumhamisha mtu katika eneo alilokaa zaidi ya miaka 20? Hivi hao wanaokadiria tjamani ya nyumba na mali zilizomo wanadhani hiki ni kipimo tosha?
Nawaza mengi na sidhani kama Mwalimu Nyerere angerudi angevumilia mateso haya wanayopata watanzania, kweli kwa hali kama hii unategemea wananchi kumshangilia kiongozi wa nchi? Kwa lipi? Mkuu wa mkoa na wa Wilaya walikuwa wapi wakati wananchi wale wakidhalilishwa? Wanafanya kazi gani viongozi hawa wa kisiasa wanaolindwa na mwavuli wa serikali? Nimefurahia Zambia kuondolewa kwa vyeo hivi visivyo na msingi ambapo nchini hapa wanapewa wale walioshindwa ubunge maeneo yao au kukosa uwaziri ili waendelee kula, wale walioenda shule wayakuwa wanauona mfumo huu maarufu kama "Klepocracy"
Wakati baba na mama wakiadhibiwa mbele ya watoto wao na Polisi waliotumwa na serikalu walioichagua huku wakiimba hadi makoo kukauka katika kampeni, viongozi hawa wametulia majumbani mwao wakipanga nchi ya kwenda kutembea kwa madai ya kutafuta uwekezaji. Huyu mwekezaji anasababisha udhalilishaji huu ametoka mbinguni? Nimesikitishwa na mwanamama aliyekuwa akilia kilio kikuu huku akitamka "Tanzania hakuna amani" x 4.
Huu ni wakati muafaka kwa wananchi kuamua wenyewe na kujionea serikali wanazozichagua na kazi wanayofanya, watanzania wanabebeshwa mizigo mizito na watu wachache wasiotambua shida ni nini, wao wakiumwa mafua tu kutibiwa Ujerumani huku wakisaini mikataba dhalimu inayowanufaisha wao na familia zao huku walalahoi wakiachwa wakiwa hawana la kufanya na kupata fedheha kama hii.
Naitazama amani yetu kwa jicho la tatu, aidha yataibuka mapigano kati ya sisi na hao wawekezaji au kati ya sisi wananchi na viongozi hawa wazembe wanaouza rasilimali zetu kila kukicha kwa kivuli cha uwekezaji. Hivi Moreno Ocampo hayaoni haya? NATO na UN hawaoni udhalilishaji huu? Mkataba wa haki za binadamu wa mwaka 1948 tuliosaini ndio unatuongoza hivi? Uko wapi umuhimu wa kuwa na makamu katibu wa UN?
Poleni sana wananchi ,mliodhalilishwa na kuonekana kama wakimbizi katika nchi yenu, mungu anasikia kilio chenu. Na huu ndio wakati muafaka kwenu kufungua macho na kufanya maamuzi sahihi 2015.

NANI ANAWAPA POLISI NGUVU YA KUPIGA RAIA NA KUHARIBU MALi ZAO? MIAKA 50 YA UHURU HAIMFAIDISHI MLALAHOI

Thursday, October 20, 2011

KILICHOMTOKEA JK UDSM NI HALALI KABISA:NCHI INANUKA

Jana majira ya saa 6:30 mchana katika chuo kikuu mlimani palitokea aibu kubwa ambayo itabaki kumbukumbu. Wanafunzi wa UDSM waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya kuwapokea Marais wawili waliokuwa wageni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 ya kitivo cha sheria chuoni hapo ambao wote ni wahitimu chuoni hapo kwa nyakati tofauti walikumbwa na aibu hiyo.
Mwenyeji wa shughuli hiyo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya muungano Mh. J.M. Kikwete akiongozana na mgeni mwalikwa ambae ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa na Rais Mstaafu Mzee AlHassan Mwinyi waliingia chuoni hapo mishale ya saa 6 mchana na mara tu baada ya kufika ndipo walipokumbwa na zomeazomea hiyo huku wanafunzi hao wakiimba ' Kama sio juhudi zako Nyerere x 3 mafisadi wangesoma wapi?'.
Naunga mkono swala hilo huku nikianza kukosoa matatizo mbalimbali ambayo serikali inayoongozwa na J.K imeshindwa kuyatatua huku mara nyingi akilalamikia watendaji wake kumkwaza, swali ni je amechukua hatua gani? Hebu jiulize alitegemea kushangiliwa na wanachuo hao kwa lipi? Kama ameshindwa kushughulikia matatizo mbalimbali yanayolikumba Taifa atashangiliwa kwa lipi?
Unawezaje kumshangilia Rais huku unakufa kwa njaa kutokana na mfumuko wa bei na kushuka kwa shilingi? Utamshangiliaje Rais huku Nishati muhimu kwa maendeleo(Umeme) umekuwa haueleweki huku yeye akicheka na wahusika? Unamshangiliaje Rais huku mikopo kwa wanavyuo ikiwa haieleweki na idadi kubwa ya wanaostahili hawapati? Huku baadhi ya vyuo kama Tumaini Dar es Salaam College kikiendelea kutoza ada kubwa mno (2.4million per year) na huduma zikiwa ni mbovu mno, wanafunzi wanasomea chini ya miti, maktaba ikiwa haina vitabu vya kutosha na matatizo ya uhaba wa wakufunzi. Wengi hawapendi kwenda pale ila wanajikuta tayari wamepangwa na bodi ya vyuo TCU Je Rais alitegemea kushangiliwa na watu wenye machungu kama hawa?
Lazima ufike wakati watanzania tuache unafiki na tumpatie kila mtu kile anachostahili, kwa lipi kati ya hayo lingemfanya ashangiliwe? Huku wanafunzi wakishindwa kulipa malipo ya hosteli kutokana na kuchelewa kwa mikopo na wakikabwa koo na mama ntilie mtaani, wana lipi la kufurahia? Nadhani hilo ni funzo tosha na kama mabadiliko yasipofanywa ategemee fedheha kubwa zaidi toka kwa wasomi ambao wanaelewa matatizo chungu nzima ya nchi hii yanayotokana na utawala mbovu.
Unawezaje kuwalipa Dowans 94bn huku Mtanzania wa kawaida akiumia na makali ya maisha kwa uzembe wa watu wawili au watatu walioingia mikataba dhalimu na ya kifisadi? Wanajulikana ila Rais amechukua hatua gani? Ifike wakati tuseme basi, nawapongeza UDSM kwa ujasiri wao na wamefungua njia.
Tuamke Watanzania

GHADDAFI ADAIWA KUKAMATWA NA MAJESHI YA NATO

Kiongozi wa zamani wa Libya anadaiwa kukamatwa na majeshi ya NATO katika mapigano yaliyokuwa yakiendelea katika jimbo la Sirte ambapo ndipo alipozaliwa kiongozi huyo.
Habari ambazo bado hazijathibitishwa rasmi na serikali ya mpito nchini humo zinasema Rais huyo wa zamani amekamatwa na ana majeraha katika miguu yake yote miwili baada ya mapambano yaliyokuwa yanaendelea katika jimbo hili. Habari hizo zimeeleza pia Waziri wa zamani wa ulinzi wa serikali ya Kanali Ghaddafi ajulikanae kama Abu Bakr Yunis amefariki dunia.
Kaa tayari kwa habari zaidi

SHAME: JK AZOMEWA NA WANAFUNZI WA UDSM

Huku hali ikiendelea kuwa tete kwa Chama Cha Mapinduzi sambamba na viongozi wake ambapo wanatafunwa na siasa za makundi, baadhi ya matukio yamekuwa yakiibuka ambapo yanawaacha watu midomo wazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya M. Kikwete amezomewa na wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam alipodhuru chuini hapo kwa kushindwa kushughulikia matatizo mbalimbali yanayowakumba wanavyuo mbalimbali nchini ikiwamo swala la mikopo sambamba na matatizo mbalumbali yanayoikumba nchi ikiwamo kushuka kwa thamani ya shilingi sambamba na kupanda kwa gharama za maisha na matatizo mengineyo likiwamo la umeme
Mambo yakiwa hayajatulia ndani ya Chama baada ya fukuto la uchaguzi wa Igunga ambapo CCM walishinda kwa tabu japo jimbo lilikuwa mikononi mwao toka mwaka 1994 chini ya Rostam Aziz, tukio jingine lililowashangaza watu ni fujo zilizoikumba UVCCM huko Arusha sambamba na kujisafisha katika vyombo vya habari kwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa huku akitishia atawashtaki wote watakaotumia jina lake vibaya katika vyombo vya habari.
Mmmmmmh hali ni mbaya kwa kweli, hii ni Tanzania tunayoitaka?

MTANGAZAJI AJITANGAZA SHOGA KWENYE TAARIFA YA HABARI

Mtangazaji wa televisheni ya ABC nchini Marekani Danny Cliff amejitangaza kuwa yeye ni shoga katika taarifa ya habari ya kituo hicho ambapo yeye ndie alikuwa msomaji.
Hali hiyo ya kushangaza iliwaacha wengi vinywa wazi kwani ni jambo ambalo hawakulitegemea, Danny ambae swala la yeye kuwa shoga lilikuwa likifahamika na ndugu na marafiki wa karibu amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kinyanyasaji vinavyowakumba baadhi ya mashoga duniani kote na akitolea mfano wa mwanafunzi mwenye miaka 14 aliyejiua huko Marekani baada ya wanafunzi wenzie kuwa wanamwandama na kumnyanyasa baada ya kujitangaza hadharani kuwa ni shoga.
Hivi karibuni ambapo shoga mmoja aliomba haki zao kutambuliwa katika jamii na katiba mpya iwafikirie kama sehemu ya jamii katika kongamano la jinsia lililoandaliwa na TGNP na pia shoga mwingine maarufu hapa nchini maarufu kama Aunt Suzy alijitangaza hadharani katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm ambapo pia baada ya hapo alipata shambulio toka kwa mwanaume aliyekuwa anaishi nae.
Tutafika kweli? Hii inaashiria nini? Je tuwatambue hawa kama moja ya wanajamii?

Tuesday, October 18, 2011

USHAURI WA BURE KWA SERIKALI

Kwa mtazamo wangu kwa hali ilivyo sasa katika eneo la Ubungo kutokana na kuwa na mitambo mingi hasa eneo la karibu na darajani ni heri wananchi wa maeneo yale wangehamishwa na kupelekwa maeneo mengine.
Kuna wafanyabiashara ambao hupanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara ya Mandela sambamba na Gereji ambayo ipo laribu kabisa na mitambo ya Aggreco ambapo kama litajitokeza tatizo kubwa zaidi ya la leo maisha ya watu wengi yanaweza kupotea, ni zaidi ya mara 6 sasa kwa uzoefu wangu toka nimehamia eneo la Ubungo kwa matatizo kama haya kutokea, au tunasubiri makibwa kama ya MV Spice ndio turekebishe?
Usipoziba ufa..................

MITAMBO MIPYA YA AGGRECO YAPATA HITILAFU KUBWA

Tanesco Tanzania wameendelea kuandamwa na mikosi na hii ni baada ya mitambo mipya iliyofungwa katika eneo la Ubungo katika wilaya ya Kinondoni ambayo ilitegemewa kupunguza mgao kupata hitilafu kubwa usiku huu muda wa saa 5 na dakika 51
Mitambo hiyo iliyokuwa katika matengenezo kwa siku kadhaa sasa ikitarajiwa ingepunguza makali ya mgao kwa kuchangia zaidi ya megawati 150 katika gridi ya Taifa imekumbwa na mkasa huo huku Tanesco wakiandamwa na balaa jingine la kesi ya Dowans na mgao usio na kikomo, tega sikio kwa habari zaidi.

Monday, October 17, 2011

LETS FIGHT AGAINST MALARIA: Miss Mtwara 2011/12 afariki dunia

Miss Mtwara mwaka 2011/12 Rahma Swai amefariki dunia kwa Ugonjwa wa malaria, mlimwende huyo ambae alikuwa moja ya washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 lililofanyika mwezi uliopita amefariki baada ya kuugua muda mfupi tu.
Mungu ailaze roho ya marehemu pema na hii ni changamoto kwetu kutumua vyandarua bila kudharau na kupima afya zetu mara kwa mara sambamba na kuwahi hospitali kila tunapojisikia vibaya.

Saturday, October 15, 2011

KADA WA CCM ATAMANI UPINZANI USHINDE MWAKA 2015: AKISAIDIA CHADEMA MRADI WA MAJI

Kada wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba zaidi ya visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa CHADEMA nchini huku akieleza angependa kuona upinzani unachukua nchi mwaka 2015.
Kada huyo maarufu wa CCM toka enzi za Mwalimu Nyerere alikuwa akipokea mpango wa uchimbaji wa visima hivyo toka kwa Katibu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa. Kauli hiyo ya Sabodo ambaye pia aliwasaidia sh100 milioni CHADEMA katika kampeni zao imekuja wakati CCM inakabiliwa na mpasuko kutokana na Siasa za makundi.
Katika mazungumzo hayo Sabodo alimhakikishia Dk Slaa kwamba ataendelea kuisaidia CHADEMA katika miradi mbalimbali inayowahusu wananchi hususani suala la Elimu na maji.
Mabadiliko yanakuja tuongeze nguvu

Friday, October 14, 2011

CHRISS BROWN ANG'AA KATIKA BET 2011 AWARDS

Jana usiku msanii alieandamwa na misukosuko miaka miwili iliyopita Chriss brown alitwaa tuzo 4 katika BET awards, miongoni mwa tuzo alizotwaa ni Best Male R&B Artist, Best Collabo song katika Look At Me Now sambamba na Lil Wayne na Busta ambapo wimbo huo pia ulishinda tuzo ya Best HipHop Video. Tuzo nyingine ni kama ifuatavyo.
MVP of the year - Nick Minaj
Made you look Award - Nick Minaji
Dj of the Year - Dj Khaled
Producer of the Year - Lex Luger
Hustler of the Year - Jay Z
CD of the Year - Kanye West & Jay Z
Best Mixtape of the Year - J. Cole
I Am Hip-Hop Icon Award - LL Cool J
New Artist of the Year - Wiz Khalifah
Track of the Year(black&yellow)-Wiz Khalifah
Best Live Perfomer & Lyricist - Lil Wayne
Perfomers where-
T.I, Lupe Fiasco, Erykah Badu, Eminen and Swizz Beats.
Its all bout entertainments

MSHINDI WA BSS APATIKANA

Hatimaye jana mshindi wa shindano la BSS Second Chance Hajji Ramadhani jana alijinyakulia 40m za BSS huku akifuatiwa na Joseph Cuthbert katika show ambayo msanii toka Uganda Navio na msanii toka Nigeria Mr. Flavor walikamua vilivyo na kuzima mbwembwe za mastaa wa Bongo. Kama ulifika hope ulieenjoy

Sunday, October 2, 2011

Saturday, October 1, 2011

http://www.mwananchi.co.tz/

Sasa unaweza soma gazeti la Mwananchi katika blog yangu, tembelea http//ronnieelmagnifico.blogspot.com