WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Saturday, December 24, 2011

CHRISTMASS GIFT: OPEN HERE

I wanna take this opportunity as the owner of this Blog/Page to wish all of my fans and friends who visit here every now & then a
MERRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012.
May GOD bless you all and make you to see another 100 Xmass Celebration. Down here its a special message to you in this Christmass eve

"People hurt you
God will heal you
People humiliate you
God will magnify you
People judge you
God will justify you"

From
Ronald Richard Makawa

Monday, December 19, 2011

MVUA YAZUA BALAA DAR ES SALAAM

Mvua iinayoendelea kunyesha ndani na nje ya jiji toka mishale ya saa kumi alfajiri zimezua balaa katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam. Mvua hizo zimesababisha baadhi ya mito jijini hapa kufurika huku mitaro ikishindwa kupitisha maji mengi yanayopita kwa kasi swala ambalo limefanya mitaro hiyo kumwaga maji njiani.
Maeneo ya Ubungo Darajani, Kibangu na Riverside yameonekana kujaa maji ambapo maji yamejaa sehemu nyingi ambapo pia maeneo ya Sinza na Tandale pia hayafai kutokana na kujaa kwa maji. Maeneo ya Manzese na Magomeni hasa eneo la Jangwani pia maji yamejaa na kuzuia barabara katika baadhi ya maeneo.
Sio maeneo hayo tu katika maeneo ya Posta, Gongo la mboto, Mbagala na Kurasini pia yamefurika jambo ambalo limesababisha kuwa na foleni kubwa jijini.
Wakazi wa mabondeni hali ni mbaya mno na juhudi za haraka zinahitajika kuwasaidia watu hawa.

TAARIFA MAALUM TOKA TANESCO

Kutokana na mvua kubwa zinazoambatana na Radi zinazoendelea katika jiji la Dar es salaam toka mishale ya saa 10 alfajiri, zimesababisha kukatika kwa umeme katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nguzo za umeme zimedondoka kama eneo la Ubungo na Tabata Segerea jambo ambalo limeilazimu Tanesco kuzima umeme baadhi ya maeneo kuepusha hatari.
Nikizungumza na moja ya wafanyakazi wa kitengo cha mawasiliano asubuhi hii ambae hakuwa tayari jina lake kuwekwa hapa amesema wananchi wanapaswa kutembea kwa makini wakati huu wa mvua na endapo utaona popote ambapo nguzo imedondoka au nyaya kukatika na matatizo mengine ya umeme toa taarifa Tanesco mara moja, ameendelea kusema katizo hili la umeme ni la muda na hali itakapokuwa shwari watashughulikia baadhi ya maeneo yenye matatizo na shughuli zitaendelea kama kawaida.
Tanesco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Friday, December 16, 2011

RATIBA YA 16 BORA UEFA YATANGAZWA: LOOK DOWN

Ratiba ya mechi za raundi ya 16 bora imetangazwa na UEFA mchana huu na ni kama ifuatavyo

Chelsea vs Napoli
Arsenal Vs AC Milan
Lyon vs Apoel Nicosia
Basel vs Bayern Munchen
Barcelona vs Bayern Leverkusen
Real Madrid vs CSKA Moscow
Inter Milan vs Marseile
Zenit St. Petersburg vs Benfica

Mechi za kwanza zitakuwa kati ta tarehe 14/15

Wednesday, December 14, 2011

BE CARE: WATU 102 WAFA KWA KUNYWA POMBE YENYE SUMU

Watu 102 wamefariki dunia baada ya kunywa pombe inayodhania kuwa na sumu aina ya Methanol katika kijiji cha Sangrampur katika jimbo la Kolkota huko India.
Akizungumzia habari hii, hakimu wa jimbo hilo amesema Narayan Swarup Nigam amesema watu hao walianza kufariki siku ya jumanne na hadi sasa watu wanne wanashikiliwa kwa tukio hilo.
Hii ni tahadhari kubwa kwa wale walevi wa pombe za kienyeji maarufu kama mataputapu ambazo hata muda mwingine tumekuwa hatujui zinatengenezwaje.

Source: BBC

MATUKIO KUMI YAKUKUMBUKWA MWAKA 2011: SOMA HAPA

Ifuatayo ni orodha ya matukio ambayo hayataweza kusahaulika katika mwaka 2011. Matukio haya yamekuwa na rekodi za kipekee jambo ambalo limefanya Blogu yako hii ya kijamii kuamua kuyaainisha tukielekea ukingoni mwa mwaka huu, matukio hayo ni kama ifuatavyo:-
1. BABU WA LOLIONDO (KIKOMBE)
Ni moja ya stori ambazo zilizagaa kila sehemu ndani na nje ya nchi hii, Babu ambae ni mchungaji Ambilikile Mwasipile aliyekuwa akitoa dawa kwa mfumo wa kikombe alifanikiwa kuwapatia zaidi ya watanzania milioni 5 dawa iliyokuwa inaaminika kutibu magonjwa mbalimbali sugu. Nani anaweza kubisha hii haikuwa habari kubwa?

2. AJALI YA FIVE STARS MODERN TAARAB
Ajali ya kundi maarufu la Taarab la Five Star Modern Taarab iliyotokea eneo la Mikumi Mkoani Morogoro, 22 March na kuua wasanii 13 wa kundi hilo ilikuwa moja ya tukio kubwa kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi yetu kwa wanamuziki wengi kiasi hicho kupoteza uhai. Mungu awalaze pema peponi

3. UCHAGUZI WA IGUNGA
Ni tukio jingine la kusikitisha katika mwaka 2011 ambapo tulishuhudia ndugu zetu wengi wakipoteza maisha katika fujo za uchaguzi huo huku pakiwa na matumizi mabaya kabisa ya pesa hasa kwa Chama tawala. Tulishuhudia matukio mengi ya udhalilishaji na uvunjifu wa haki za binadamu jambo ambalo lilichafua sifa ya Taifa hili. Mungu azilaze roho za mashujaa waliofariki wakipigania haki

4. JAIRO SKENDO
Ni miongoni mwa habari zilizopewa kipaumbele mno katika mwaka 2011 ambapo katibu huyu wa wizara ya nishati na madini alizichangisha taasisi 20 zilizochini ya wizara hiyo milioni hamsini kila moja kwa ajili ya kuhonga ili bajeti mbovu ya wizara yao ipitishwe. Swala hilo linaingia kwenye orodha hii kwa kuwa ni jambo jipya masikioni mwetu na ni ufujaji wa pesa za umma huku maamuzi ya kurejeshwa kwake kazini na kuondolewa tena ilikuwa kitendawili pia.

5. MISAADA YENYE MASHARTI YA KUUKUBALI USHOGA
Ni kauli iliyowaacha wengi vinywa wazi toka kwa Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron dhidi ya nchi zilizochini ya Jumuiya ya Madola ambapo alizitaka nchi hizo kuzitambua hali za mashoga na wasagaji katika jamii kama kigezo cha misaada. Aliendelea kwa kudai watakaokiuka wasingepatiwa misaada jambo ambalo lilipingwa ba wengi.

6. KIFO CHA OSAMA BIN LADEN NA MUAMMAR GHADAFI
Hawa ni watu wawili tofauti walioitikisa dunia kwa matukio tofauti, vifo vyao vilizua mjadala mkubwa ambapo wengi hawakuamini juu ya vifo vya miamba hii. Tukianza na Osama Bin Laden ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda aliuawa mwezi wa 5 huko Pakistan na kifo chake kuzua utata mkubwa baada ya mwili wake kutoonyeshwa huku Ghadafi akiuawa mwezi 10 na wapiganaji Wa NATO sambamba na waasi wa nchi hiyo.

7. AJALI YA MELI HUKO NUNGWI
Ni ajali inayofananishwa na ile ya MV Bukoba iliyotokea mwa 1996 ambapo maelfu ya watu walipoteza maisha. Katika ajali hii ya meli ya MV Spice ilishuhudia watu zaidi ya 250 kwa mujibu wa serikali walipoteza maisha kutokana na ajali hiyo ya kizembe.

8. MILIPUKO YA MABOMU GONGO LA MBOTO
Ni miongoni mwa tukio lililotokea mwaka huu na kuanza majonzi makubwa baada ya mabomu yaliyokuwa yamehifadhila katika maghala ya kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto. Watu zaidi ya 500 walijeruhiwa vibaya katika milipuko hiyo, wengine zaidi ya 30 wakipoteza maisha na makazi ya watu zaidi ya 5000 yaliharibiwa.

9. KUJIVUA GAMBA
Ni moja ya kauli ambazo haziwezi kuondoka midomoni mwa watu kirahisi, hii ilikuwa kauli mbiu toka kwa CCM ambapo ilikuwa ikiwataka viongozi wa Chama hicho wenye kashfa kujiuzulu ambapo 14 Jully mbunge wa Igunga Rostam Aziz alijivua gamba huku wengine wakigoma na baadae swala hilo kusitishwa na Rais baada ya Mh. Lowasa kuja juu na kumwaga mboga........ Simo

10. MATUMIZI MAKUBWA KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU NA SWALA LA POSHO
9 dESEMBA mwaka huu ilikuwa ni siku ya kuadhimimisha miaka 50 toka nchi hii kupata uhuru wake, tulishuhudia sherehe kubwa za kuonyesha ufahari huku nchi ikiwa katika orodha ya nchi masikini za kutupwa ambapo tupo katika nafasi ya 152 kati ya nchi 189 zinazoendelea na nchi ya tatu kwa kupatiwa misaada baada ya nchi zenye vita za Iraq na Afghanstan. Katika sherehe hizo fedha zinazokadiriwa kufikia sh 64 bilioni zilitumika. Sina mengi ya kusema juu ya hilo na swala la mwisho ambalo utata wake unaendelea ni posho za wabunge zinazotakiwa kupandishwa na kuwa shilingi laki 3 na 30 kwa kikao ambazo ni shilingi 80 za kujikimu, shilingi 50 za mafuta na posho kwa siku ambayo ni laki mbili.
Mungu ibariki Tanzania

Source: Ronald Richard Library
Tanzania Newspapers
Jamii Forum
Online search Engines

Tuesday, December 13, 2011

5 FACTS ABOUT FACEBOOK USERS IN tANZANIA

Facebook is a social networks that links and create friendship and networking to many people worldwide, but some of illiterate people start to misuse it and label it as a place to show how foolish the're. Below are five facts about Facebook friends in Tanzania.

1. Fake reality is the first fact for friends in Facebook, many of them fake they are names, pics and relationship status, be care with them and take 10% only of people's profiles.

2. Distortion is the second fact, take only few of what they post otherwise you will destroy your mind with foolish & nonsense, how can someone post naked or half naked pics of him/her? And when people ask him/her, he/she end up by saying dats me, be care friend

3. Exploitation of Sex and Manipulation is another fact where some of bums & nuts are here to destroy others reputation and respect infront of others. If your love leaves you here is not a right place to tell us what happen, reality stays there your nothing thats why he/she leaves you. To send his/her naked pics or tell her abusive words is not the solution

4. Murder of character is another fact about facebook friends in Tanzania where some of foolish people open an account for the sake of destroy others reputation bya telling lies and wrong facts about other. Its better if you open an Taarab Band and speak your nonsense there.

5. Illiteracy is the last fact about facebook friends of Tanzania, a lot of people they dont know what to post and at which time, not all the time we are there to Joke and sometimes its important to stay quite instead of writting shits. You must have a claim that is supported by reasons and evidence its how you can write well. Most people in Facebook listen a half, understanding only quarter of what they hear and speak a lot. Be carefull with selection of friends. Its better to have ten real friends than having 500 fake & foolish friends.
Mark my words, if you go somewhere with nine foolish people know that your number ten of them, friends reflects who you are and some of people sees you from your friend.

Friday, December 9, 2011

MISAMIATI 30 ILIKOSA MAJIBU KATIKA MIAKA 50 YA UHURU

Hii ni orodha ya maneno ambayo yamekosa maana ya moja kwa moja na yametesa sana vichwa vya watanzania.
1. Kuchakachua
2. Mchakato
3. Uwekezaji
4. Posho
5. Katiba
6. Maisha bora kwa kila mtanzania
7. Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya
8. Megawati
9.Kujivua Gamba
10. Hadidu za rejea
11. Barabara za juu
12. Mabasi ya mwendo kasi
13. upembuzi yakinifu
14. Sharobaro
15. Fursa sawa kwa wote
16. Richmond
17. EPA
18. Rasimu
19. Kamati teule
20. Tume ya uchunguzi
21. Mfumuko wa bei
22. Muafaka
23. Maslahi ya umma
24. Utandawazi
25. Ruksa
26. Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele
27. Wahisani
28. Kichwa cha mwenda wazimu
29. Haki za Binadamu
30. Mafisadi

Wewe kama mtanzania mwenzangu hebu changia ulichoelewa katika misamiati hii.

Thursday, December 8, 2011

VIBAKA WAMFANYIA KITU MBAYA DIAMOND

Yule mkali wa bongo anaetesa na kibao cha Mawazo kwa sasa baada ya kusumbua na vibao kadhaa kama vile Moyo wangu, Nitarejea na Mbagala, Diamond Platinum a.k.a Baba Wema juzi akitokea kwenye shughuli za kurekodi video yake mpya ya mawazo alipaki gari yake nje ya sehemu anapoishi na alipoingia ndani tu jamaa wenye vyao wakakomba vitu kibao
Akizungumza kwa huzuni, Diamond amesema miongoni mwa vitu vilivyochukuliwa ni pamoja na power window zote, radio, system ya AC na begi lililokuwa na nguo, cheni kibao za gold na saa nyingi alizokuwa akizitumia katika kushoot video yake mpya ya mawazo.
Pole sana mtu mzima

Tuesday, December 6, 2011

HIVI RAIS YUPO AU AMESAFIRI? NCHI INAONGOZWA NA NANI?

Naukumbuka wimbo mmoja wa taarab unaimbwa "Jahazi likikosa nahodha chombo huenda mrama". Haya ndiyo yanayoendelea sasa hapa nchini. Mambo makubwa mengi yanatokea na kiongozi wa nchi yupo kimya tueleweje?
Tanesco wanampango wa kuongeza umeme mara tatu na hatujaona kauli yoyote toka kwa kiongozi wa nchi kama akivyoahidi ataboresha maisha ya wananchi. Posho zimepandishwa na kwa ujumla sasa mbunge atakuwa akipewa 330,000 kwa siku atakapohudhuria kikao kimoja cha bunge kima ambacho ni mshahara wa mwalimu anaeanza kazi.
Hivi kwa mtindo huu tunategemea maandamano yapungue au kuisha? Maisha yapo juu na mfumuko wa bei umekuwa juu sambamba na kushuka kwa thamani ya shilingi, tulitegemea Rais angetoa tamko la jinsi ya kudhibiti haya yote ila imekuwa kinyume kabisa.
Wananchi inapaswa tuamke sasa na tuchukue hatua, hivi palikuwa na haja gani ya kutumia mamilioni yote hayo kusherekea miaka 50 ya Uhuru? Inamnufaisha nini mwananchi wa kawaida? Miaka 50 ya uhuru ni kwa ajili ya viongozi wanaojiongezea mishahara kila wanapojisikia na ingekuwa heri kama wananchi wangezisusia sherehe hizi za kinafki.
Nchi imeshika nafasi ya tatu kwa kupewa misaada duniani na ya kwanza Afrika, nafasi ya juu kwa rushwa na miongoni mwa nchi 50 maskini zaidi duniani. Kwa mtindo huu kazima tulazimishwe kuukubali ushoga ili tupewe misaada. Tafakari, chukua hatua.....

Saturday, December 3, 2011

TUNDAMAN APATA AJALI MBAYA

Msanii maarufu wa kundi la Tiptop Connection maarufu kwa jina la Tundaman au Mikidadi amepata ajali mbaya ya gari akiwa njiani toka Kahama kuelekea Shinyanga kwa ajili ya Shoo.
Tundaman amesema chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na kuchoka kwa dereva ambae alianza kusinzia na kusababisha gari yao aina ya Toyota Cresta kupinduka kichwa chini miguu juu.
Katika safari hiyo Tundaman aliongozana na Dj Kman(wa kundi la Tiptop) na dereva ambae alifariki papo hapo. Hali zao zinaendelea vizuri na mungu awape afya njema

Friday, December 2, 2011

MAKUNDI YA EURO 2012 YATANGAZWA. LOOK DOWN

Makundi ya michuano ya Euro 2012 itakayofanyika huko Poland & Ukraine yametangazwa. Makundi hayo ni kama ifuatavyo
Group A
Poland, Greece, Russia, Czech Republic
Group B
Holland, Denmark, Germany, Portugal
Group C
Spain, Italy, Republic of Ireland, Croatia
Group D
Ukraine, Sweden, France, England
Katka makundi yote kundi B ndilo linaonekana gumu zaidi katika michuano ambao inaonekana itakuwa yakuvutia.

Thursday, December 1, 2011

MR EBBO AFARIKI DUNIA

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipyaAbell Motika maarufu kama Mr Ebbo amefariki dunia huko mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo.
Msanii huyo maarufu ambae enzi za uhai wake alitamba na nyimbo kama Mi mmasai, maneno mbofumbofu, kamongo na mnisamehe huku akighani kwa staili ya kimasai amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi. Msanii huyo pia alikuwa mmiliki wa studio ya Motika Records.
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahala pema peponi.