Mashabiki 74 wamepoteza maisha yao jana mjini Port Said nchini Misri katika mchezo uliozikutanisha timu za Al Masry dhidi ya timu inayoongoza ligi kuu nchini humo ya Al Ahly ambapo timu hiyo ndogo ya Al Masry ilifanikiwa kuifunga timu ya Al Ahly kwa jumla ya magoli 3 - 1.
Baada ya filimbi ya mwisho mashabiki wa timu mwenyeji ya Al Masry walivamia uwanja na kuanza kuwakimbiza wachezaji wa Al Ahly na kuwapiga ambapo katika fujo hizo wachezaji kadhaa wa Al Ahly walijeruhiwa na Polisi walifanikiwa kuingilia kati na kuwaokoa.
Wengi wa mashabiki hao wamefariki kutokana na kukanyagana na wengine kwa majeraha walipokuwa wakipigana na mashabiki wa timu pinzani.
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter amesema amesikitishwa sana na tukio hilo ambalo halitegemewi kutokea katika soka mara nyingi na ana majonzi kwa wale waliopoteza ndugu zao kutokana na tukio hilo na kusema kwa kifupi "It was a black day in Footbal"
Chama cha soka nchini humo kimetangaza kusimamisha michezo ligi ya mpira kwa muda usiojulikana wakati huu ambapo uchunguzi unaendelea huku pakiwa na dalili kwa timu ya Al Masry kufutwa katika ulimwengu wa soka.
Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi.
Source: SkySports Football Website
www.skysports.com
KIBAHA KUANZA KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA
31 minutes ago

No comments:
Post a Comment