Magoli mawili yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji wa Barcelona raia wa Chile Alexis Sanchez sambamba na goli murua toka kwa mchezaji bora wa dunia kwa mara tatu mfululizo Lionel Messi yamewapa Barcelona ushiindi mnono wa magoli 3 ~ 1 dhidi ya Bayern Leverkusern ya Ujerumani na kujihakokishia nafasi ya kucheza katika hatua ya robo fainali.
Barcelona ambayo ilikuwa ugenini walitangulia kupata goli katika dakika ya 41 likifungwa na Sanchez ila Bayern wakafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Kadlec aliyemalizia krosi murua ya Corluka, bao hilo lilidumu kwa muda mfupi ambapo Barca waliongeza goli la pili dakika ya 54 likifungwa na Sanchez tena baada ya kugongewa pasi murua na Fabregas na Messi akihitimisha la 3 dakika za mwishoni. Kwingineko mabingwa wa zamani wa Ufaransa Olympic Lyonas walijipatia ushindi mwembamba wa goli
1 ~ 0 dhidi ya Apoel Nicousia ya Urusi kupitia kwa Alexandre Lazerette baada ya kumbabatiza mlinzi wa timu hiyo ya Urusi na mpira uliojaa kimiani. Ushindi kwa timu hizo mbili zikiwa ugenini ni dalili nzuri ya kuffuzu kwa hatua inayofuata.
Kesho patakuwa na michezo mingine kati ya Arsenal vs AC Milan na CSKA Moscow vs Real Madrid.
MRADI WA TACTIC KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA
50 minutes ago
No comments:
Post a Comment