WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Saturday, October 29, 2011

MAKALI YA MGAO WA UMEME KUREJEA UPYA: WAZIRI WA FEDHA AGOMA KUTOA FEDHA ZA UNUNUZI WA MAFUTA KWA IPTL

Mgao wa umeme ambao ulisitishwa kwa muda na serikali baada ya kuamua kutoa fedha ajili ya ununuzi wa mafuta kwa kampuni ya IPTL kwa mwezi Agosti na Septemba unaelekea kurejea baada ya Waziri wa Fedha Mh Mustafa Mkullo kugoma kutoa fedha hazina kwa ajili ya zoezi hilo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Mkullo alisema "Sema kabisa kwamba Waziri wa Fedha kasema wizara yake haihusiki na malipo hayo", aliendelea kwa kusema serikali haiwezi kutumia hela za walipa kodi kuyapatia makampuni yaliyoajiriwa na Tanesco ajili ya kuzalisha umeme.
Kampuni ya IPTL inachangia kiasi cha Megawati 80 katika gridi ya Taifa na kama itashindwa kuzalisha kiwango hicho hii inamaanisha makali ya mgao yatarejea kama awali, msemaji wa Tanesco Badra Masoud amesema shirika hilo linatumia zaidi ya bilioni 17 kwa mwezi ajili ya ununuzi wa mafuta kiasi ambacho ni kikubwa mno kwao na kusitishwa huko kwa fedha kutaiingiza nchi kwenye mgao mkali tena.
Aliongeza kuwa kiwango cha maji kwa sasa katika bwawa la Mtera ni kidogo kuzingatia kiwango cha 690mm ambacho ndio sahihi kwa ajili ya kuzalisha nishati hiyo ila wameiombwa Wizara ya maji na wamewakubalia kuanza shughuli hiyo huku akisema hata kukatika kwa umeme mara kwa mara kunatokana na matatizo hayo.
Mgao wa umeme ulipungua makali yake baada ya makampuni ya Symbion 37megawati, IPTL megawati 80 na AGGreko 75megawati kuchangia kiasi cha Megawati 192 katika gridi ya Taifa. Tujiandae ma mgao kwa kweli.
Hii ndio Tanzania

No comments:

Post a Comment