WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Thursday, October 20, 2011

KILICHOMTOKEA JK UDSM NI HALALI KABISA:NCHI INANUKA

Jana majira ya saa 6:30 mchana katika chuo kikuu mlimani palitokea aibu kubwa ambayo itabaki kumbukumbu. Wanafunzi wa UDSM waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya kuwapokea Marais wawili waliokuwa wageni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 ya kitivo cha sheria chuoni hapo ambao wote ni wahitimu chuoni hapo kwa nyakati tofauti walikumbwa na aibu hiyo.
Mwenyeji wa shughuli hiyo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya muungano Mh. J.M. Kikwete akiongozana na mgeni mwalikwa ambae ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa na Rais Mstaafu Mzee AlHassan Mwinyi waliingia chuoni hapo mishale ya saa 6 mchana na mara tu baada ya kufika ndipo walipokumbwa na zomeazomea hiyo huku wanafunzi hao wakiimba ' Kama sio juhudi zako Nyerere x 3 mafisadi wangesoma wapi?'.
Naunga mkono swala hilo huku nikianza kukosoa matatizo mbalimbali ambayo serikali inayoongozwa na J.K imeshindwa kuyatatua huku mara nyingi akilalamikia watendaji wake kumkwaza, swali ni je amechukua hatua gani? Hebu jiulize alitegemea kushangiliwa na wanachuo hao kwa lipi? Kama ameshindwa kushughulikia matatizo mbalimbali yanayolikumba Taifa atashangiliwa kwa lipi?
Unawezaje kumshangilia Rais huku unakufa kwa njaa kutokana na mfumuko wa bei na kushuka kwa shilingi? Utamshangiliaje Rais huku Nishati muhimu kwa maendeleo(Umeme) umekuwa haueleweki huku yeye akicheka na wahusika? Unamshangiliaje Rais huku mikopo kwa wanavyuo ikiwa haieleweki na idadi kubwa ya wanaostahili hawapati? Huku baadhi ya vyuo kama Tumaini Dar es Salaam College kikiendelea kutoza ada kubwa mno (2.4million per year) na huduma zikiwa ni mbovu mno, wanafunzi wanasomea chini ya miti, maktaba ikiwa haina vitabu vya kutosha na matatizo ya uhaba wa wakufunzi. Wengi hawapendi kwenda pale ila wanajikuta tayari wamepangwa na bodi ya vyuo TCU Je Rais alitegemea kushangiliwa na watu wenye machungu kama hawa?
Lazima ufike wakati watanzania tuache unafiki na tumpatie kila mtu kile anachostahili, kwa lipi kati ya hayo lingemfanya ashangiliwe? Huku wanafunzi wakishindwa kulipa malipo ya hosteli kutokana na kuchelewa kwa mikopo na wakikabwa koo na mama ntilie mtaani, wana lipi la kufurahia? Nadhani hilo ni funzo tosha na kama mabadiliko yasipofanywa ategemee fedheha kubwa zaidi toka kwa wasomi ambao wanaelewa matatizo chungu nzima ya nchi hii yanayotokana na utawala mbovu.
Unawezaje kuwalipa Dowans 94bn huku Mtanzania wa kawaida akiumia na makali ya maisha kwa uzembe wa watu wawili au watatu walioingia mikataba dhalimu na ya kifisadi? Wanajulikana ila Rais amechukua hatua gani? Ifike wakati tuseme basi, nawapongeza UDSM kwa ujasiri wao na wamefungua njia.
Tuamke Watanzania

No comments:

Post a Comment