Ifuatayo ni orodha ya matukio ambayo hayataweza kusahaulika katika mwaka 2011. Matukio haya yamekuwa na rekodi za kipekee jambo ambalo limefanya Blogu yako hii ya kijamii kuamua kuyaainisha tukielekea ukingoni mwa mwaka huu, matukio hayo ni kama ifuatavyo:-
1. BABU WA LOLIONDO (KIKOMBE)
Ni moja ya stori ambazo zilizagaa kila sehemu ndani na nje ya nchi hii, Babu ambae ni mchungaji Ambilikile Mwasipile aliyekuwa akitoa dawa kwa mfumo wa kikombe alifanikiwa kuwapatia zaidi ya watanzania milioni 5 dawa iliyokuwa inaaminika kutibu magonjwa mbalimbali sugu. Nani anaweza kubisha hii haikuwa habari kubwa?
2. AJALI YA FIVE STARS MODERN TAARAB
Ajali ya kundi maarufu la Taarab la Five Star Modern Taarab iliyotokea eneo la Mikumi Mkoani Morogoro, 22 March na kuua wasanii 13 wa kundi hilo ilikuwa moja ya tukio kubwa kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi yetu kwa wanamuziki wengi kiasi hicho kupoteza uhai. Mungu awalaze pema peponi
3. UCHAGUZI WA IGUNGA
Ni tukio jingine la kusikitisha katika mwaka 2011 ambapo tulishuhudia ndugu zetu wengi wakipoteza maisha katika fujo za uchaguzi huo huku pakiwa na matumizi mabaya kabisa ya pesa hasa kwa Chama tawala. Tulishuhudia matukio mengi ya udhalilishaji na uvunjifu wa haki za binadamu jambo ambalo lilichafua sifa ya Taifa hili. Mungu azilaze roho za mashujaa waliofariki wakipigania haki
4. JAIRO SKENDO
Ni miongoni mwa habari zilizopewa kipaumbele mno katika mwaka 2011 ambapo katibu huyu wa wizara ya nishati na madini alizichangisha taasisi 20 zilizochini ya wizara hiyo milioni hamsini kila moja kwa ajili ya kuhonga ili bajeti mbovu ya wizara yao ipitishwe. Swala hilo linaingia kwenye orodha hii kwa kuwa ni jambo jipya masikioni mwetu na ni ufujaji wa pesa za umma huku maamuzi ya kurejeshwa kwake kazini na kuondolewa tena ilikuwa kitendawili pia.
5. MISAADA YENYE MASHARTI YA KUUKUBALI USHOGA
Ni kauli iliyowaacha wengi vinywa wazi toka kwa Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron dhidi ya nchi zilizochini ya Jumuiya ya Madola ambapo alizitaka nchi hizo kuzitambua hali za mashoga na wasagaji katika jamii kama kigezo cha misaada. Aliendelea kwa kudai watakaokiuka wasingepatiwa misaada jambo ambalo lilipingwa ba wengi.
6. KIFO CHA OSAMA BIN LADEN NA MUAMMAR GHADAFI
Hawa ni watu wawili tofauti walioitikisa dunia kwa matukio tofauti, vifo vyao vilizua mjadala mkubwa ambapo wengi hawakuamini juu ya vifo vya miamba hii. Tukianza na Osama Bin Laden ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda aliuawa mwezi wa 5 huko Pakistan na kifo chake kuzua utata mkubwa baada ya mwili wake kutoonyeshwa huku Ghadafi akiuawa mwezi 10 na wapiganaji Wa NATO sambamba na waasi wa nchi hiyo.
7. AJALI YA MELI HUKO NUNGWI
Ni ajali inayofananishwa na ile ya MV Bukoba iliyotokea mwa 1996 ambapo maelfu ya watu walipoteza maisha. Katika ajali hii ya meli ya MV Spice ilishuhudia watu zaidi ya 250 kwa mujibu wa serikali walipoteza maisha kutokana na ajali hiyo ya kizembe.
8. MILIPUKO YA MABOMU GONGO LA MBOTO
Ni miongoni mwa tukio lililotokea mwaka huu na kuanza majonzi makubwa baada ya mabomu yaliyokuwa yamehifadhila katika maghala ya kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto. Watu zaidi ya 500 walijeruhiwa vibaya katika milipuko hiyo, wengine zaidi ya 30 wakipoteza maisha na makazi ya watu zaidi ya 5000 yaliharibiwa.
9. KUJIVUA GAMBA
Ni moja ya kauli ambazo haziwezi kuondoka midomoni mwa watu kirahisi, hii ilikuwa kauli mbiu toka kwa CCM ambapo ilikuwa ikiwataka viongozi wa Chama hicho wenye kashfa kujiuzulu ambapo 14 Jully mbunge wa Igunga Rostam Aziz alijivua gamba huku wengine wakigoma na baadae swala hilo kusitishwa na Rais baada ya Mh. Lowasa kuja juu na kumwaga mboga........ Simo
10. MATUMIZI MAKUBWA KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU NA SWALA LA POSHO
9 dESEMBA mwaka huu ilikuwa ni siku ya kuadhimimisha miaka 50 toka nchi hii kupata uhuru wake, tulishuhudia sherehe kubwa za kuonyesha ufahari huku nchi ikiwa katika orodha ya nchi masikini za kutupwa ambapo tupo katika nafasi ya 152 kati ya nchi 189 zinazoendelea na nchi ya tatu kwa kupatiwa misaada baada ya nchi zenye vita za Iraq na Afghanstan. Katika sherehe hizo fedha zinazokadiriwa kufikia sh 64 bilioni zilitumika. Sina mengi ya kusema juu ya hilo na swala la mwisho ambalo utata wake unaendelea ni posho za wabunge zinazotakiwa kupandishwa na kuwa shilingi laki 3 na 30 kwa kikao ambazo ni shilingi 80 za kujikimu, shilingi 50 za mafuta na posho kwa siku ambayo ni laki mbili.
Mungu ibariki Tanzania
Source: Ronald Richard Library
Tanzania Newspapers
Jamii Forum
Online search Engines
WELCOME
MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED
BE BLESSED
MY DIARY
- RONALDTHEGREAT
- Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
- FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE
RONNIE DOCOMENTARY
-
▼
2011
(157)
-
▼
December
(13)
- CHRISTMASS GIFT: OPEN HERE
- MVUA YAZUA BALAA DAR ES SALAAM
- TAARIFA MAALUM TOKA TANESCO
- RATIBA YA 16 BORA UEFA YATANGAZWA: LOOK DOWN
- BE CARE: WATU 102 WAFA KWA KUNYWA POMBE YENYE SUMU
- MATUKIO KUMI YAKUKUMBUKWA MWAKA 2011: SOMA HAPA
- 5 FACTS ABOUT FACEBOOK USERS IN tANZANIA
- MISAMIATI 30 ILIKOSA MAJIBU KATIKA MIAKA 50 YA UHURU
- VIBAKA WAMFANYIA KITU MBAYA DIAMOND
- HIVI RAIS YUPO AU AMESAFIRI? NCHI INAONGOZWA NA NANI?
- TUNDAMAN APATA AJALI MBAYA
- MAKUNDI YA EURO 2012 YATANGAZWA. LOOK DOWN
- MR EBBO AFARIKI DUNIA
-
▼
December
(13)
Popular Posts
-
Beckham akishangilia goli lililoiondoa Argentina katika 16bora za World Cup 2002 Beckhamakimpa moyo David Seaman baada ya kuondoshwa na...
-
Kada wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba zaidi ya visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa CHADEMA nchini huku akieleza angependa k...
-
Animals are such agreeable friends – they ask no questions, they pass no criticisms.”
-
Notorious B.I.G. AKA Christopher G. Wallace Born: 21-May - 1972 Birthplace: Brooklyn, NY Died: 9-Mar - 1997 Location of death: Los A...
-
Polisi mkoani Arusha leo alfajiri katika muda wa saa kumi na moja wamevamia katika viwanja vya NMC na kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA walioua...
-
AKITOA TAARIFA JUU YA MASULUHISHO HAYO MSANII WA KUNDI LA WAGOSI WA KAYA AMESEMA:KWANZA POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTO...
-
Arshavin amejiunga na klabu yake ya zamani ya Zennit Petrsburg ya Urusi kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu, mchezaji huyo ambae alikuwa akiip...
OTHER BLOG LIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment