WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Tuesday, November 1, 2011

TUNATAKIWA KUUKUBALI USHOGA ILI TUONGEZEWE MISAADA: SHINIKIZO TOKA SERIKALI YA UINGEREZA

Serikali ya Uingereza imezitaka nchi zinazoendelea kuzitambua haki za mashoga la sivyo zitapunguziwa ama kuondolewa kabisa misaada inayotolewa na nchi hiyo.
Kauli hiyo kali na yakusikitisha imetolewa na Waziri wa Uingereza anaeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Andrew Mitchel alipokuwa akizungumzia misaada inayotolewa Afrika. namnukuu " We'll cut your aid if you persecute gays". Ametoa kauli hiyo ikiwa tayari serikali yake imeiondolea nchi ya Malawi £19million baada ya kuwahukumu kifungo cha miaka 14 mashoga Tiwangole Chimbalanga 26 na Steven Monjeza 20 waliovalishana pete ya uchumba hadharani.
Waziri huyo pia ametishia kuzipunguzia misaada Uganda inayopata £70million kila mwaka na Ghana £36million toka nchini humo kwakuwa wamekuwa wakipinga ushoga bila woga. Msemaji wa Waziri huyo pia alitoa kauli kali katika kusisitiza hilo akisema " Serikali yetu imejipanga kuhakikisha kuwa vitendo vya kihalifu na unyanyasaji dhidi ya mashoga, wasagaji, watu wenye jinsia mbili na walipandikizwa jinsi tofauti na walizozaliwa nazo vinadhibitiwa na haki zao kutambuliwa katika jamii ndani na nje ya Uingereza" aliendelea kusisitiza akisema "Sasa tutaelekeza misaada yetu kwa wale watakaozingatia hili na tutakuwa tukitoa misaada kila baada ya miezi mitatu na sio kwa mwaka mzima kama ilivyokuwa awali jambo ambalo litatuwezesha kupitia kwa umakini kufuatwa kwa haki hizo. Tutaelekeza misaada ya moja kwa moja pale tutakaporidhika kuwa nchi za Afrika zinafuata masharti yetu ya kupunguza umaskini na kuheshimu haki za binadamu".
Swali linabaki kwetu, Je tupo tayari kuukubali ushoga ili tupatiwe misaada? Tungoje kuona viongozi wetu hasa mkubwa wa nchi kama atatoa kauli kuhusiana na hili. Tayari hapo juzi serikali hiyo ya Uingereza ilitishia kutupunguzia $490million katika bajeti yetu kwa kuwa hatutimizi yale wanayoyataka, hebu wayaainishe basi ili tuelewe. Tuwe makini na tulipinge hili kwa nguvu moja. Shime Watanzania, hii sio sawa mbele za Mungu, tusiogope kutopatiwa misaada.

No comments:

Post a Comment