MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE. BE BLESSED
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MIGOMO NA MAANDAMANO VYUO VIKUU. Serikali imeonya kwamba haitavumilia na kutishia kufuta uhamini wa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini watakaoshiriki kwenye migomo na maandamano kwa sababu zisizo na msingi. Msimamo huo ulitolewa mapema wiki hii na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dk. Shukuru Kawambwa alipozungumza na jamii ya Chuo kikuu cha Tumaini Makumira wakati wa ziara ya kujifunza shughuli, utendaji na changamoto zinzovikabili vyuo vikuu nchini. Alisema msimamo huo wa Serikali unaotokana na dhamira ya kuboresha mfumo wa elimu ya juu nchini uliosababisha wizara yake kutengewa 300 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
No comments:
Post a Comment