WELCOME
MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED
BE BLESSED
MY DIARY
- RONALDTHEGREAT
- Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
- FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE
RONNIE DOCOMENTARY
-
▼
2012
(43)
-
▼
February
(35)
- MANDELA IN "SATISFACTORY CONDITION" AFTER OPERATION
- ARSHAVIN, SAMBA WAKIMBILIA RUSSIA
- ARSENAL & TOTTENHAM ZAONYA MASHABIKI WAKE
- WARAKA WA SIRI TOKA KWA MH. HARRISON MWAKYEMBE
- SUGU NA RUGE WAPATANISHWA
- SITTA - MWAKYEMBE KALISHWA SUMU, POLISI WANAPOTOSHA
- WIZARA YA AFYA YAMRUKA DCI MANUMBA:NI KUHUSU TAARI...
- ASAMOAH GYAN QUITS INTERNATIONAL FOOTBALL
- TAARIFA YA DKT HARRISON MWAKYEMBE KUJIBU KAULI YA ...
- WENGER TO SELL WALCOTT & OTHER 5 PLAYERS IN SUMMER...
- MAJAMBAZI YAVAMIA ENEO LA MLIMANI CITY
- MATOKEO YA MICHEZO YOTE YA EUROPA ILIYOFANYIKA JAN...
- HABARI ZILIZOPAMBA MAGAZETI YA SOKA ULAYA LEO
- HONDURAS: FIRE KILLS 300 PRISONERS IN JAIL
- KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED KITAKACHOIVAA AJAX KA...
- HABARI ZILIZOPEWA KIPAUMBELE MAGAZETI YA SOKA ULAY...
- ARSENAL KUVAA JEZI TOFAUTI LEO DHIDI YA AC MILAN
- BARCA, LYON ZAANZA VIZURI 16 BORA UEFA
- FA TO PUNISH SUAREZ
- R.I.P: WHITNEY HOUSTON 48 DIED
- WONDERFUL: PROSTITUTES IN LUSAKA OFFER FREE SEX FO...
- TAARIFA TOKA TANESCO JUU YA MGAO UNAOENDELEA
- YALIYOAMULIWA KUHUSU MADAI YA MADAKTARI:MASHARTI W...
- The list is compiled by gathering income streams f...
- MCHANGANUO WA MATOKEO KIDATO CHA NNE: DARAJA LA KW...
- WACHORA PICHA, KUANDIKA MATUSI NA VERSE ZA BONGO F...
- FABIO CAPELLO RESIGNED TO COACH ENGLAND
- UTAFITI: NUSU YA WANAUME NCHINI NI WAGUMBA
- TAARIFA MAALUM KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TOKA JUKW...
- KAULI NA MSIMAMO WA MBUNGE jOHN MNYIKA KUHUSU MGOM...
- MADAKTARI BINGWA MUHIMBILI WAGOMA RASMI
- BARIDI INAYOENDELEA ULAYA YAUA 300
- YASEMAVYO MAGAZETI YA SOKA ULAYA LEO.
- TERRY APOKONYWA UNAHODHA ENGLAND
- MASHABIKI 74 WAFARIKI KATIKA FUJO MISRI
-
▼
February
(35)
Popular Posts
-
A massive fire has swept through a jail in Honduras, killing at least 300 prisoners, officials say. Many victims were burned or suffocated t...
-
The 5,000 sq ft home includes a saltwater pool, glassed in sunroom, outside fireplace, 5 bedrooms and 5 baths ... but no apparent grotto,...
-
PFA chief executive Gordon Taylor believes it is time for the FA to intervene after Luis Suarez and Patrice Evra failed to shake hands befor...
OTHER BLOG LIST
Tuesday, February 21, 2012
WARAKA WA SIRI TOKA KWA MH. HARRISON MWAKYEMBE
AUSAMBAZA KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKE WA KARIBU NAIBU Waziri wa Ujenzi anayeugua ugonjwa uliozusha utata mkubwa serikalini, Dk. Harrison Mwakyembe, ameandika waraka mahususi unaoeleza kile anachokiamini kuwa ni chanzo cha ugonjwa wake, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Waraka huo ambao gazeti hili limeuona mbali ya kueleza kile ambacho Mwakyembe mwenyewe anaamini kuwa ni chanzo cha ugonjwa wake, unaeleza pia jinsi alivyoanza kuugua, watu anaowashuku kuwa nyuma ya mpango huo, siku na tarehe aliyodhani kuwa ndiyo aliyowekewa sumu hiyo. Kama hiyo haitoshi, Mwakyembe katika waraka wake huo pasipo kueleza chanzo halisi cha undani wa taarifa zake, anaeleza mbinu iliyotumika kumdhuru na mahala mpango huo wa kumdhuru ulipopangwa. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba Dk. Mwakyembe ambaye kwa sasa yuko nchini India ameusambaza waraka huo kwa ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu. Katika waraka huo, Dk. Mwakyembe anaeleza kwamba anaamini alipewa sumu hiyo akiwa ofisini kwake huku akitaja majina ya watu anaowatuhumu kuwa nyuma ya mpango huo ambao gazeti hili kwa sasa linahifadhi majina yao. Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, mara tu baada ya kuwekewa sumu hiyo alianza kuwashwa mwili kabla ya hali kuendelea kuzorota na kuwa mbaya. Akionekana kujibu hoja za Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, mwanasiasa huyo katika waraka wake anaeleza kwamba hakuwekewa sumu hiyo kwenye chakula, bali kwenye sabuni na kitaulo cha kujifutia, ambacho huwekwa kwenye chumba maalumu ofisini kwake kwa ajili ya kusafisha mikono na huduma nyingine awapo ofisini. Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa ndugu na marafiki wa karibu wa Dk. Mwakyembe vilisema kuwa, naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, amefikia hatua ya kuandika waraka huo kwa lengo la kutaka kuijulisha familia yake na taifa kile anachoamini anakabiliana nacho endapo atapoteza maisha kabla ya ukweli kamili kubainishwa. Hata hivyo, kutokana na ukweli kwamba suala hilo la afya ya Dk. Mwakyembe liko katika hatua za uchunguzi, Tanzania Daima Jumatano haliwezi kuandika kwa undani kuhusu waraka huo kwa sasa. Ukiacha hilo, Dk. Mwakyembe katika waraka huo ameelezea historia ya maisha yake kisiasa na mikasa iliyompata kiasi cha kujijengea maadui.Ameeleza jinsi alivyonusurika kuuawa mara kadhaa na kwamba taarifa zote za mikasa yake aliziripoti polisi, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na Jeshi hilo la Polisi. Baadhi ya mikasa aliyoitaja kwenye waraka huo ni pamoja na tukio la kunusurika kuuawa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mei 21, mwaka 2009. Ajali hiyo ilitokea eneo la Ihemi, kilomita 40 kutoka Iringa mjini akiwa safarini kutokea Mbeya kwenda Dar es Salaam. Kwa mujibu wa waraka huo, gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Land Cruiser T 362 ACH, liliacha njia saa moja asubuhi baada ya kukanyaga shimo na tairi ya upande wa kulia kuchomoka na dereva wake, Joseph Msuya (30), kupoteza mwelekeo kabla ya gari hilo kutoka nje ya barabara upande wa kushoto na kuparamia mti kisha kupinduka. Ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Dk. Mwakyembe akijaribu kulipita lori kabla ya kukanyaga shimo hilo. Anasema katika ajali hiyo aliokolewa na wasamaria wema pamoja na trafiki wawili waliokuwa kwenye basi dogo waliokuwa wakisafiri kutoka Iringa kwenda Njombe. Anasema katika waraka huo kuwa, baada ya ajali hiyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kutokana na kuumia taya kisha alihamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Kwa mujibu wa waraka huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, aliunda tume iliyoongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati huo, Kamanda James Kombe, kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Matokeo yalionesha kwamba ilisababishwa na uzembe wa dereva wake, Msuya wakati Dk. Mwakyembe akiamini kwamba ajali hiyo ilipangwa.Februari 9, mwaka 2011, Dk. Mwakyembe aliandika barua kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, akimpa taarifa juu ya kuwapo kwa njama za kutaka kumuua yeye pamoja na viongozi wengine. Wengine aliowataja katika barua hiyo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela. Katika orodha hiyo ya Mwakyembe kwa IGP, hadi sasa kiongozi mwingine ambaye anaumwa ni Profesa Mark Mwandosya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment