WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Tuesday, February 7, 2012

UTAFITI: NUSU YA WANAUME NCHINI NI WAGUMBA

UTAFITI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini ni wagumba ukipingana madai ya wengi kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake.Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya mwaka 2009 na Septemba 2010 unaonyesha, asilimia 47.05 ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba.Malengo ya utafiti huo uliosimamiwa na Dk Henry Mwakyoma, yalikuwa ni kubaini ni kwa kiasi gani wanaume huweza kuathiriwa katika via vyao vya uzazi na hatimaye kushindwa kutungisha mimba. Utafiti huo ulionyesha kati ya wanaume 221 waliopimwa, asilimia 30.03 walikuwa na mbegu dhaifu na asilimia 17.02 walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu. Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Dk Mwakyoma alisema, ugumba kwa wanaume limekuwa tatizo sugu katika miaka ya hivi karibuni. “Nasisitiza kuwa, pengine mwanaume aliwahi kupata watoto hapo awali, lakini sasa hivi hapati, bado atakuwa mgumba,” alisema Dk Mwakyoma.Alisema hapo awali ilikuwa vigumu kupata idadi kamili ya wanaume wenye ugumba kwa sababu walikuwa hawajitokezi kupima.“Angalau sasa hivi wanakuja na tunawapima, ingawa ni kazi ngumu kuwapa majibu yao,” alisema Mwakyoma. Sababu za ugumba Mwakyoma alitaja sababu za ugumba kwa wanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii. Alitaja sababu nyingine kuwa ni kemikali zinazoingia katika miili yetu, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo. Dk Mwakyoma aliongeza kuwa, wanaoathirika zaidi ni wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda mrefu.“Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanaume, kubeba laptop, unene kupita kiasi na mazingira,” alisema. Dk Mwakyoma akifafanua jinsi kitengo chake kinavyopima manii ili kujua kama zina matatizo au zipo salama, alisema, " rangi ya mbegu pamoja na umbile huangaliwa ili kutambua ubora wake. Hata kwa kuziangalia tu, mbegu zenye rangi aidha kijivu au nyeupe si salama.” Kwa upande wake, Dk Innocent Mosha, ambaye ni daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Muhimbili alisema, wamefanikiwa kupata takwimu hizo kutokana na wanandoa wengi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kujua sababu ya kutokuwa na watoto katika ndoa yao."Mara nyingi matokeo huonyesha tatizo liko kwa mwanaume. Lakini kuna tabu ya kuwaeleza ukweli, wengi hawataki kukubali," alisema Dk Mosha. Aliongeza, “Kesi kama hizo huleta migogoro ya kifamilia, kwani huenda mwanamke huyo amekwishamzalia mumewe watoto ambao kimantiki si wa kwake,” alisema Dk Mosha. Dk Mosha alisema, kuna ugumba wa aina mbili; wa kuzawa nao na ugumba unaopatikana ukubwani. “Wapo wanaozaliwa na ugumba, yaani mbegu zao aidha ni dhaifu au hawana kabisa mbegu tangu kuzaliwa kwao,” alisema Dk Mosha. Shirika la Afya duniani (WHO) linathibitisha kuwa, ujazo wa manii anaopaswa kuwa nao mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni milligram moja na nusu hadi nne na nusu na kuongeza, “Ujazo wa manii ukipungua au ukizidi basi mbegu hizo zina matatizo” alisema Dk Mwakyoma. Naye Dk Joshua Noreh wa kituo cha upandikizaji cha jijini Nairobi (IVF centre) alisema, tatizo la ugumba alianza kuliona tangu mwaka 2006 baada ya kupokea wanandoa wengi kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania waliofika kutafuta huduma ya upandikizaji wa mbegu ili kupata watoto. Utafiti uliofanywa na WHO mwaka 2009 duniani, ulibainisha kuwa, mwanaume mmoja kati ya saba wanaofika kupima afya ya uzazi hugundulika na matatizo ya ugumba.

No comments:

Post a Comment