WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Wednesday, February 22, 2012

ARSENAL & TOTTENHAM ZAONYA MASHABIKI WAKE

Timu za soka zinazotokea katika jiji la London na zilizo katika Big 4 ya ligi kuu ya England zimewaonya mashabiki wake kujiepusha na vitendo vya kibaguzi katika kuelekea mchezo mkali kabisa utakaozikutanisha timu hizo siku ya jumapili.
Katika mchezo huo Mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Emmanuel Adebayor atakuwa akirejea kwa mara ya kwanza toka ajiunge na Tottenham Hotspurs kwa mkopo akitokea Manchester City. Adebayor ambae anatarajia mapokezi mabaya katika uwanja wa Emirates amekuwa katika kiwango bora kabisa msimu huu mara baada ya kutolewa kwa mkopo kwa Real Madrid msimu uliopita na sasa akiichezea Tottenham ambapo katika mcchezo uliopita ambao Tottenham iliifunga timu ngumu ya Newcastle 5 - 0, Adebayor alihusika katika utengenezaji wa magoli manne na yeye kufunga moja.
Kauli toka kwa klabu hizo imekuja mara baada ya Waziri mkuu wa England Mh David Cameron kutoa karipio kali juu ya vitendo vya kibaguzi katika soka hapo jana katika mkutano dhidi yake na chama cha soka cha Uingereza FA, Cameron alisema kama jambo hilo lisiposhughulikiwa kwa ufasaha litaurudisha mchezo wa soka nyuma katika miaka ambapo ubaguzi ulishamiri.

No comments:

Post a Comment