WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Tuesday, January 31, 2012

USAJILI DIRISHA DOGO ENGLAND

Usajili uliokamilika kwa timu za Uingereza
Everton -Nikica Jelavic toka Rangers
Tottenham - Louis Saha toka Everton
QPR - Djibril Cisse(Lazio) Bobby Zamora(Fulham)
Fulham - Pavel Pobrebynyak (Sturtgatt)
Westham - Ravel Morrison(Man Utd)
Manchester United - Vessel (Man City)
Manchester City - David Pizzaro (Roma)

Monday, January 30, 2012

HATIMAYE INTER WARIDHIA KUMUUZA SNEIJDER MANCHESTER: ASAFIRI KUPIMWA AFYA USIKU HUU

Timu ya Inter Milan ya nchini Italia imeridhia kumuuza kiungo mshambuliaji wa timu hiyo kwa ada ya £25m. Wesley Sneijder ambae amekuwa akiwindwa na Mashetani wekundu kwa muda mrefu sasa anatarajiwa kusafiri usiku huu kwa vipimo vya afya jijini Manchester na baadae atatangazwa rasmi kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa.

Habari zaidi baadae
From Official source

Monday, January 23, 2012

BALOTELI AMALIZIA HASIRA ZAKE KWA HARRY REDNAPP:AMCHAFUA KATIKA TWITTER

Baada ya mchezaji mtukutu wa club ya Manchester City kufungiwa michezo minne na chama cha soka nchini Uingereza FA. Ameendeleza visa vyake kwa kupost picha ya katuni ya kocha huyo wa Tottenham yenye picha ya mbwa usoni na trend yenye maneno
#MyDogAteMyTaxReturns.
Hii imekuja baada ya kocha huyo kupeleka mashtaka FA baada ya mchezo wa jana. Harry anakabiliwa na kesi ya kukwepa kulipa kodi alipokuwa kocha wa Portsmouth ambapo alifungua akaunti benki aliyoipa jina la mbwa wake.
Kuicheki katuni hiyo tembelea akaunti ya twitter ya mchezaji huyo yenye jina la @MarioBalotelAd.

BALOTELI AFUNGIWA MECHI NNE

Chama cha soka nchini Uingereza kimetangaza hukumu ya kumfungia Mchezaji wa Manchester City Mario Baloteli kutokana na kitendo chake cha kumpiga teke usoni Mchezaji wa Tottenham Hotspurs Scott Parker katika mchezo wa jana.
Akizungumza kwa masikitiko msemaji wa FA Gramne Souness amesema "I think he should sent off" huku akiongeza kuwa " mguu wake wa kulia ulipaswa kutangulia mbele baada ya kuupiga mpira ila kitendo cha kuurudisha nyuma kilikuwa cha makusudi. Kufuatia tukio hilo Baloteli atakosa mchezo wa marudiano wa Carling Cup dhidi ya Liverpool na michezo mitatu ya ligi dhidi ya Everton, Fulham na Aston Villa, hukumu hiyo inatarajowa kuanza mara moja na endapo wakikata rufaa FA anaweza kucheza mchezo dhidi ya Liverpool na uchunguzi wa FA ukirudiwa anaweza kuongezewa adhabu.
Gramne Souness pia alimshangaa mwamuzi Howard Webb kwa kutompatia kadi ya pili ya njano mchezaji huyo ambayo ingemtoa nje ya mchezo huku akisema " Great players are consistent, but Baloteli is a car crush waiting to happen

Wednesday, January 18, 2012

THIERRY HENRY APATA MAJERAHA MAZOEZINI

Nyota wa Klabu ya New York Redbulls ya Marekani aliye katika kikosi cha Arsenal kwa mkopo wa miezi miwili amepata majeraha katika mazoezi asubuhi ya leo jambo ambalo linaweza kumuweka nje katika mchezo wa jumapili dhidi ya Manchester United.
Henry(34) alitua katika klabu yake hiyo ya zamani mwanzoni mwa mwezi huu na amecheza michezo miwili hadi sasa dhidi ya Leeds United na Swansea City akiwa amepachika goli moja tayari.

Thursday, January 12, 2012

AJIKATA UUME NA KUCHOMA NYUMBA MOTO

Mkazi mmoja wa kijiji cha Nyamakendo anafahamika kwa jina la Maregei Werema amejikata sehemu kubwa ya uume wake na kuuacha ukining'inia sambamba na kuteketeza kwa moto nyumba zake mbili na mali zilizokuwamo ndani.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Mara Robert Boaz alisema Bw Werema alifanya matendo hayo tarehe 11 January baada ya kupandwa na malaria kichwani ambapo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya DDH - Mugumu.
Malaria haikubaliki jamani, ukihisi dalili tu wahi mapema kituo cha afya kupima na kupata tiba sahihi ili yasikukute kama haya

Tuesday, January 10, 2012

MAANDALIZI YA BONANZA LA MICHEZO YA TUMAINI YAENDELEA

Mikocheni campus team
Timu ya  mpira wa miguu ya wavulana ya chuo cha Tumaini tawi la mikocheni inajiandaa kwa ajili ya michezo maalum ya chuo inayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 14 January 2012. timu hiyo inaundwa na wanafunzi wa kozi zote katika tawi la mikocheni.


Monday, January 9, 2012

DIAMOND AHUKUMIWA MIEZI 6 JELA

Msanii Naseeb Abdul maarufu kama Diamond amehukumiwa kwenda Jela miezi 6 na mahakama ya mwanzo mkoani Iringa kwa kosa la kuharibu vifaa vya mwandishi wa habari aliyekuwa akimhoji.
Habari zaidi baadae