Hatimaye serikali kupitia Wizara ya Mali Asili na Utalii imetoa namba maalum ambazo zitawawezesha watanzania kuupigia kura mlima Kilimanjaro uweze kuingia katika maajabu mapya saba ya dunia.
Zoezi hilo ambalo lilizinduliwa toka Julai mwaka huu limekuwa la kusuasua na ni baada ya njia pekee ya kuupigia kura mlima huo ikiwa ni kwa njia ya mtandao ambapo ni idadi ndogo tu ya watanzania wenye uwezo wa kufanikisha zoezi hilo kutokana na wengi kutojua jinsi ya kufanya ama kutokuwa na mawasiliano hayo ambayo mara nyingi yanahusisha kompyuta.
Zikiwa zimesalia siku 10 pekee zoezi hilo kukamilika Wizara hiyo imetangaza namba hizo ni 15771 kwa mitandao ya Vodacom, Tigo, Sasatel na Zantel na namba 15021 kwa wateja wa Airtel.
Wazo hilo ambalo katibu wa Wizara hiyo amelipata kwa kijana mdogo ambae hakutaka kumtaja katika mazungumzo yake na waandishi wa Habari jambo ambalo libaonesha viongozi wetu ni wavivu kufikiri. Amesema hadi sasa ni asilimia 20% pekee ya watanzania waliopiga kura huku akihamasisha watanzania kuupigia mlima huo kura za kutosha.
Ili kuweza kupiga kura unatakiwa kutuma neno KILIMANJARO kwenda namba 15771 kwa VODACOM, TIGO, SASATEL & ZANTEL na namba 15021 kwa wateja wa AIRTEL.
Shime Watanzania tuupigie kura mlima wetu kuuingiza katika rekodi hizo.
WAZIRI DKT. GWAJIMA AZINDUA MAHABUSU YA WATOTO MTWARA
53 minutes ago
No comments:
Post a Comment