WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Thursday, February 9, 2012

YALIYOAMULIWA KUHUSU MADAI YA MADAKTARI:MASHARTI WALIYOTOA

Haya ndiyo baadhi ya yaliyoamuliwa kuhusu madai ya Madaktari Kwa ufupi, kutoka kwa watu waliokuwemo kwenye mkutano wa Madaktari na Waziri Mkuu katika ukumbi wa CPL, Muhimbili, haya ndiyo yaliyotatuliwa: Pendekezo kuwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamii kuondoshwa katika nafasi zao limefanikiwa nusu kwani Waziri Mkuu amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Peniel Lyimo kuwaandikia barua za likizo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu, Dkt. Deo Mtasiwa il hali Waziri Haji Hadji Mponda na Naibu Waziri Dkt. Lucy Nkya watasubiri maamuzi ya Rais Kikwete. Nyongeza ya "Call Allowances" inaanza mara moja mwezi huu. Watalipwa ifuatavyo: Specialist MDs (25,000/=), Regular MDs (20,000/=); AMO, COs (15,000) Registered Nurses (10,000/=) na baada ya bajeti kutakuwa na mabadiliko ambapo mafao haya yataangaliwa upya. Kimeundwa Kikosi Kazi vha watu 9 chenye Daktari mmoja kwa ajili ya majadiliano na kutoa maamuzi juu ya mshahara pamoja na "allowances" zote (Nyumba, House allowances, Hardship allowances nk). Kikosi kazi kina muda wa wiki mbili kufanya kazi hii. Usafiri: Madaktari watapewa mikopo ya magari Green Card kwa kila Daktari na familia yake inaanza mara moja. Kwa hivyo, Madaktari wameazimia kuahirisha mgomo na kurudi kazini ili kuwahudumia Watanzania. Madaktari watakutana tena rasmi kufanya tathmini ya maamuzi yote ya sasa na ya Kikosi Kazi hapo tarehe 3 Machi 2012. Waziri Mkuu aliruhusu mikutano ya Madaktari aliyoizuia awali kufanyika, na ndipo Madaktari walipopata fursa ya kuendelea kukutana na kujadiliana baada ya mkutano wao na Waziri Mkuu kumalizika.

No comments:

Post a Comment