Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC) imegundua ufisadi wa kutisha uliokuwa unafanyika ndani ya Bodi ya TCRA iliyo chini ya Jaji Buxton Chipeta. Akizungumzia swala hilo bwana Deo Filikijombe ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge inayoshughulikia matumizi ya mashirika ya umma alisema pesa nyingi zilizoorodhesha katika taarifa ya matumizi ya bodi hiyo zimetumika kifisadi na pakiwa na mazingira ya wazi ya ubadhilifu wa pesa za umma.
Miongoni mwa matumizi hayo ni shilingi
bilioni 2.2 zilizotumika kusomesha watendaji watatu wa mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka 2009/10 na kwa ujumla mpaka mwaka huu bodi hiyo imetumia bilioni 4.1 kwa ajili ya kugharamia mafunzo kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo, swali la kujiuliza ni kwamba hawa waliogharimiwa mabilioni haya mbona mchango wao katika jamii? Wanafunzi wengi wa Vyuo vikuu wanakosa mikopo ambayo ingewawezesha kusoma jambo ambalo lingechangia kuongeza idadi ya wasomi nchini. Watanzania wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku, wapi zinapatikana pesa hizi za kuwalipia vigogo hawa? Zinatoka mfuko gani?
Matumizi mengine ya kifisadi yaliyopingwa na (POAC) ni pamoja na shilingi milioni 36 zinazodaiwa kutumika kuwalipa wafanyakazi saba wa ofisi za uhasibu za mamlaka hiyo wanaodaiwa kufanya kazi muda wa ziada, dola
2,000 sawa na shilingi 3.4 milioni ambazo hutumika ajili ya mawasiliano ya bodi hiyo kwa mwezi, pia wafanyakazi wa bodi hiyo walipatiwa simu za mkononi kila mmoja zenye thamani ya dola 600 kila moja sawa na shilingi milioni 1 na wajumbe wa bodi hiyo wamekuwa wakilipwa dola 350 kila mwezi sawa na shilingi 600,000.
Filikijombe amesema kamati hiyo inashangwazwa kwanini wafanyakazi hao walipwe kwa dola baada ya shilingi? Huku akiainisha kuwa malipo ya dola 350 kwa mwezi sio sahihi kwao sababu wao sio watendaji wa kila siku wa mamlaka hiyo pamoja na dola 2,000 za mawasiliano.
Matumizi mengine ya mamlaka hiyo ni sambamba na kutumika kwa shilingi 45 bilioni katika ujenzi wa jengo hilo tofauti na ile iliyotajwa mwanzo ya shilingi 27 bilioni, pia pesa nyingine ni shilingi 600 milioni zilizotumika kwa manunuzi ya samani mbalimbali katika ofisi hizo.
Akijibu tuhuma hizo mwanasheria wa TCRA Elizabeth Nzagi amesema sio kweli kuwa mamlaka hiyo imekiuka taratibu za matumizi ya fedha za umma, akitetea kuwa mafunzo ya mambo ya mawasiliano ni gharama kubwa ndio maana wametumia 4.1 bilioni katika kipindi hicho na kwamba sio kweli kati ya hizo bilioni 2.2 zilitumika kusomesha wafanyakazi watatu kwa mwaka akidai kuna makosa ya kihasibu, swali linakuja tena hapa, inamaana hawakuisoma hiyo taarifa kabla ya kuiwakilisha? Au waliandikiwa?. Kuhusu milioni 36 zilizotumika kuwalipa wafanyakazi saba waliofanya kazi muda wa ziada amedai ni kutokana na uchache wa wafanyakazi, swali la kujiuliza wasomi wangapi wanahaha mitaani kutafuta ajira? Au hawana sifa?
Huu ni mtihani na hebu wenzangu mnaowaza mbali tazameni sinema hii mara mbili kisha mtoe tathimini, na cha kishangaza hakuna hatua zitakazochukuliwa zaidi ya kuunda tume.
Nchi imeoza, inanuka Rushwa na Ufisadi
WELCOME
MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED
BE BLESSED
MY DIARY
- RONALDTHEGREAT
- Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
- FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE
RONNIE DOCOMENTARY
-
▼
2011
(157)
-
▼
November
(29)
- MANCHESTER UNITED WATUPWA NJE:CARLING CUP
- BREAKING NEWS; WANNE WAFA KWA AJALI UBUNGO
- 26th Nov; BAADHI YA WASANII WATAKAOTUMBUIZA ; okoa...
- KUNA UMUHIMU GANI KWA KATIBA YETU KUANDIKWA KWA LU...
- URAIS 2015 WAWACHANGANYA WENGI:TABIRI ZA MASANGOMA...
- HOW TO STOP MASTERBATION ADDICTION
- MOTO MKUBWA WALIPUKA MITAMBO YA UMEME UBUNGO:MITAM...
- BREAKING NEWS: MAFURIKO DAR NA MWANZA
- NCHINI INANUKA:MNADHIMU MKUU WA JWTZ AKAMATWA NA I...
- FROM MOVENPICK TO DAR ES SALAAM SERENA HOTEL:KWELI...
- HIVI NDIVYO ALIVYOLAKIWA PRINCE CHARLES
- POLISI YAWATAWANYA WAFUASI WA CHADEMA ARUSHA
- LADY GAGA ATWAA TUZO 4 ZA MTV EUROPE MUSIC AWARDS
- JESHI LA TANZANIA LAKAMATA WANAJESHI 20 WA CONGO N...
- JESHI LA TANZANIA LAKAMATA WANAJESHI 20 WA CONGO N...
- HUDUMA ZA MAKAMPUNI YA SIMU NCHINI NI MBOVU MNO, T...
- MISS VENEZUELA IVIAN SARCOS ATWAA TAJI LA MISS WOR...
- CHURCH OF ENGLAND OPPOSED TO SAME SEX CIVIL PARTNE...
- EID MUBARAK GREETINGS ALL MUSLIMS: READ THIS
- RAIS KIKWETE AMTEMBELEA VENGU HOSPITALI
- THE MAGICIAN PAGE: KAULI YA DAVID CAMERON YAWAVIMB...
- KAULI YA DAVID CAMERON YAWAVIMBISHA KICHWA MASHOGA TZ
- BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AIPINGA KAULI YA MEMBE:...
- MLIMA KILIMANJARO KAMWE HAUWEZI KUSHINDA KWA STAIL...
- WAZIRI WA MAMBO YA NJE ATOA KAULI JUU YA MISAADA Y...
- 2.2 BILIONI ZATUMIKA KUWASOMESHA WATATU TCRA NJE K...
- RAIS WA GHANA AIKATAA MISAADA TOKA UINGEREZA YENYE...
- NAMBA ZA KUUPIIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO ZATOLEWA...
- TUNATAKIWA KUUKUBALI USHOGA ILI TUONGEZEWE MISAADA...
-
▼
November
(29)
Popular Posts
-
Beckham akishangilia goli lililoiondoa Argentina katika 16bora za World Cup 2002 Beckhamakimpa moyo David Seaman baada ya kuondoshwa na...
-
Kada wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba zaidi ya visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa CHADEMA nchini huku akieleza angependa k...
-
Animals are such agreeable friends – they ask no questions, they pass no criticisms.”
-
Notorious B.I.G. AKA Christopher G. Wallace Born: 21-May - 1972 Birthplace: Brooklyn, NY Died: 9-Mar - 1997 Location of death: Los A...
-
Polisi mkoani Arusha leo alfajiri katika muda wa saa kumi na moja wamevamia katika viwanja vya NMC na kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA walioua...
-
AKITOA TAARIFA JUU YA MASULUHISHO HAYO MSANII WA KUNDI LA WAGOSI WA KAYA AMESEMA:KWANZA POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTO...
-
Arshavin amejiunga na klabu yake ya zamani ya Zennit Petrsburg ya Urusi kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu, mchezaji huyo ambae alikuwa akiip...
OTHER BLOG LIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment