WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Friday, November 4, 2011

MLIMA KILIMANJARO KAMWE HAUWEZI KUSHINDA KWA STAILI HII: VIONGOZI WETU WENGI WAZEMBE KUFIKIRI

Tanzania kwa mara ya kwanza tumepata bahati ya moja ya vivutio vyetu vya Utalii na moja ya lebo ya Taifa mlima Kilimanjaro kutajwa kuingia katika mchujo wa kupigiwa kura unaovihusisha zaidi ya vivutio kumi duniani vikitakiwa kubaki saba ambavyo vitatangazwa kama maajabu saba mapya ya dunia.
Tunakila sababu ya kusema kwamba hii ni bahati ya pekee sio tu kwa Tanzania bali kwa nchi za Afrika Mashariki kwani kama yangeandaliwa mazingira mazuri ambayo yangewawezesha watanzania wengi kuupigia kura mapema huenda swala hili lingefanikiwa.
Kwa wale wenye mtazamo kama wangu naamini watakubaliana na mimi kwamba ni ngumu kwa mlima Kilimanjaro kuingia katika maajabu hayo mapya kwa kigezo cha kura
kwa kuwa hadi sasa ni watanzania wachache tu waliopiga kura hii inatokana na maandalizi mabovu kwa wale waliokuwa wakiratibu zoezi hilo ambalo litakamilika Novemba 11 mwaka huu.
Zoezi hilo ambalo lilizinduliwa mapema mwezi Julai mwaka huu limekosa msisimko sambamba na uhamasishaji duni toka kwa wahusika waliokabidhiwa shughuli hiyo huku siku za awali njia pekee ya kuweza kuupigia kura Mlima huo ikiwa ni kwa njia ya mtandao jambo ambalo ni gumu kwa Watanzania wengi na hii ni kokana na kuwa na miundombinu duni ya huduma hiyo na wengi wa wananchi kutofahamu matumizi ya kompyuta.
Zikiwa zimesalia siku takribani kumi Wizara ya Mali Asili na Utalii ndio wanaonekana kushtuka toka usingizini na kurahisisha zoezi hilo ambapo sasa wananchi wanaweza kuupigia kura mlima huo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu(SMS) kwa kuandika neno KILI kwenda 15771.
Maswali ya kujiuliza ni, Je watendaji hawa hawakuliona hili mapema na kutambua hii ndio njia rahisi ambayo ingewawezesha wanachi wengi kukamilisha zoezi hilo? Watendaji hawa wanafanya kazi kwa manufaa ya Taifa kweli? Watanzania wangapi wenye uelewa na matumizi ya mtandao?
Na kuwa wa kwanza kuamini ni ngumu kwa mlima wetu kuingia katika maajabu hayo kwani hadi sasa idadi ya wlioupigia kura hawazidi aslimia 20% ya watanzania wote. Hawa nao wanapaswa kuwajibishwa kwa kuwa wazembe wa kufikiri na nikiamini lazima kuna fedha zilitengwa ajili ya kushughulika na uhamasishaji wa kura ila zimetafunwa na wachache wasiofanya kazi kwa manufaa ya Taifa. Mtakubaliana na kauli hii baada ya matokeo.
Hii ndio Tanzania

No comments:

Post a Comment