Rais wa Ghana John Evans Atta Mills amekuwa kiongozi wa kwanza toka Africa kutoa kauli ya kutoikubali misaada toka UK yenye masharti ya kutambua haki za mashoga na wasagaji.
Mills amejibu moja kwa moja kuwa hawatakubali msaada wowote wenye masharti ya kukubaliana na Ushoga kama serikali ya UK chini ya David Cameron na Waziri wake wa Maendeleo ya kimataifa Andrew Mitchel ilivyotoa masharti.
Aliongeza kwa kusema Ghana ni nchi huru na haipaswi kupangiwa na Uingereza nini cha kufanya kwa kigezo cha misaada na akasema nchi ya Ghana haitaruhusu Ushoga wala kutambua haki zozote wanazopatia watu hao.
Tunahitaji viongozi kama hawa kwa kweli na tunangoja kuona Rais wetu atatoa kauli gani juu ya swala hili. Ghana inapata £36million toka UK kila mwaka.
UJENZI BWAWA LA BILIONI 2 LAKAMILIKA.
13 hours ago

No comments:
Post a Comment