Mwanamuziki wa kike mwenye vituko nchini Marekani Lady Gaga jana usiku alifanikiwa kunyakuwa tuzo nne katika tuzo zinazoandalia na ktuo cha Televisheni cha MTV.
Shindano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Odyssey Arena jijini Belfast lilikuwa zuri ambapo moja ya vituko vilivyotokea kwenye show hiyo ni mwanaume mmoja ambae alipanda stejini akiwa uchi kabisa. Tuzo alizotwaa Gaga ni:-
Mwimbaji bora wa kike
Video bora
Wimbo bora
Kipenzi cha mashabiki.
Tuzo hizo zulitanguliwa na ishara ya heshima ya kumbukumbu ya mwanamuziki Amy Winehouse ambae alikutwa amekufa ndani kwake jijini London mwezi wa saba mwaka huu.
Wengine waliong'ara katika tuzo hizo ni sambamba na Justin Bieber na Bruno Mars ambao wote walinyakua tuzo mbili kila mmoja.
Source: BBC
TUME YA MADINI YAFUNGUA FURSA KWA VIJANA
16 minutes ago

No comments:
Post a Comment