WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Sunday, November 6, 2011

HUDUMA ZA MAKAMPUNI YA SIMU NCHINI NI MBOVU MNO, TCRA WASHINDWA KUTATUA TATIZO

Huduma za mawasiliano ya simu nchini zimeendelea kuwa za mbovu mno kwa miaka kadhaa sasa huku mamlaka inayoshughulikia swala zima la mawasiliano (TCRA) ikionekana ikiwa kimya bila kutoa tamko lolote.
Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo sasa inakadiriwa watuaji hao wanafikia milioni 21, kwa mwaka 2010 pekee watumiaji wa simu za mikononi nchini waliongezeka kwa asilimia 20 huku idadi ikionekana kuongezeka kwa kasi kubwa.
Makampuni mengi ya simu za mikononi yamekuwa yakihangaika kwa kila namna kuongeza wateja kwa kuweka huduma mbalimbali huku wakitumia fedha nyingi kujitangaza. Wateja wengi wamekuwa wakiilalamikia mitandao hiyo ambayo mingi kwa sasa imeingia latika mfumo wa kibenki ambapo kuna huduma mpya nyingi za kuhifadhi fedha kupitia simu za mikononi ambapo wakati mwingine imewawia tabu kutoa au kutuma fedha kutokana na matatizo ambayo TCRA wameyafumbia macho.
Makampuni hayo ya simu za mkononi kwa sasa wamevimba kichwa kutokana na mafanikio wanayoendelea kupata na kuwasahau wateja wanaowahudumia ambapo baadhi ya makampuni haya kwa sasa yanatoza pesa kwa ajili ya simu za huduma kwa wateja jambo ambalo ni kinyume na TCRA ACT 1993.
Mamlaka hiyo ya mawasiliano imeonekana kama mbwa asiye na meno ambapo hadi sasa hakuna hatua yoyote wala tamko lililotolewa juu ya tatizo hili ambalo liko wazi kabisa. Moja ya kampuni hizo imekuwa ikitangaza kutoa gharama kwa bei nafuu huku wakikata pesa zaidi ya ile wanayotangaza huku simu zikiingia na kutoka kwa tabu na wakati mwingine kujibiwa namba haipatikani japo simu inakuwa hewani, huku wateja wake siku za karibuni wakilalamikia mfumo wa kibenki wa mtandao huo ambapo wapo wateja waliokatwa kati ya shilingi 20 hadi 1480 katika akaunti zao bila maelezo yoyote yanayoeleweka.
Swala linaloonekana sasa makampuni hayo yamekuwa yakishindana zaidi katika kuongeza idadi ya wateja na kuwekeana mipaka ya kibiashara(tarrif) ambapo ni gharama kubwa mno kupiga mtandao mmoja kwenda mwingine, huku ikionekana dhahiri kuwa makampuni hayo yameshindwa kabisa kuboresha huduma kwa wateja wao, kutokana na miundombinu ya mawasiliano hayo ikiwa ni ya kizamani na baadhi kuzidiwa na idadi ya wateja ambao wamekuwa hawana pakupeleka malalamiko yao. TCRA wanaonekana kuwa usingizini na wakiwa hawajafanya utafiti wowote juu ya huduma wanazopatiwa wateja toka walipopewa jukumu hilo.

No comments:

Post a Comment