WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Thursday, November 17, 2011

KUNA UMUHIMU GANI KWA KATIBA YETU KUANDIKWA KWA LUGHA YA KIINGEREZA?

Napata wakati mgumu jinsi ya kuandika makala hii, nagundua bado viongozi wetu wengi wana utumwa wa kifikra, hivi ipi ni lugha ya Taifa!!? Kiswahili na Kiingereza? Kwanini tunashindwa kuiheshimu na kuithamini lugha yetu? Hizi ndizo sababu hata shilingi yetu imekuwa ikiporomoka kila siku na gharama za maisha kuzidi kuongezeka sababu wapo viongizi na makampuni ambayo hadi sasa wanalipa au kulipwa kwa dola ndani ya nchi hii, bodi ya TCRA ilikuwa mfano tosha, tuachane na haya
Nashindwa kuelewa kama huo muswada wa katiba unaoleta utata bungeni kama uliandikwa hapa nchini au kwa Cameron!!!
Swali jingine gumu ninalokosa jibu lake kuna nini ndani ya muswada huo wanaokataa kuuweka katika lugha ya Taifa? Mpaka lini tutaendelea kunyenyekea lugha za wenzetu huku tukiongea kinafki kuwa kiswahili ni lugha ya Taifa?
Watanzania wangapi wenye uelewa fasaha wa lugha ya kiingereza? Hata wale wachache waliofanikiwa kupata elimu ya sekondari na elimu ya juu bado lugha hii ni changamoto kwao. Hivi hii katiba wanaandikiwa kina nani? CCM wana ajenda gani ya siri juu ya katiba hii? Siungi mkono wanachofanya CHADEMA kwa sasa bungeni ila ndio njia pekee ya kuonyesha kutoridhishwa na udikteta wa chama tawala.
Wapo baadhi ya wabunge wanapenda kuonekana wema mbele ya Rais na mwenyekiti wao wa chama wamekuwa wakisimama bungeni na kuzungumza upuuzi ambao nawaza bado wananchi wao ndicho walichowatuma? Ufike wakati tuzungumze ukweli na kuacha siasa za kishabiki, hili ndilo tatizo lililofanya wananchi wengi wa kawaida kutoielewa katiba ya zamani hadi sasa.
Patolewe machapisho mengi ya muswada huo wananchi wengi wapate kuelewa nini kinazungumziwa, katiba sio kwa ajili ya chama au wabunge, ni ya wananchi wote. Tuache umbumbumbu wa fikra, mawazo sahihi huja kwa lugha sahihi na inayoeleweka kwa wengi

No comments:

Post a Comment