WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Tuesday, December 6, 2011

HIVI RAIS YUPO AU AMESAFIRI? NCHI INAONGOZWA NA NANI?

Naukumbuka wimbo mmoja wa taarab unaimbwa "Jahazi likikosa nahodha chombo huenda mrama". Haya ndiyo yanayoendelea sasa hapa nchini. Mambo makubwa mengi yanatokea na kiongozi wa nchi yupo kimya tueleweje?
Tanesco wanampango wa kuongeza umeme mara tatu na hatujaona kauli yoyote toka kwa kiongozi wa nchi kama akivyoahidi ataboresha maisha ya wananchi. Posho zimepandishwa na kwa ujumla sasa mbunge atakuwa akipewa 330,000 kwa siku atakapohudhuria kikao kimoja cha bunge kima ambacho ni mshahara wa mwalimu anaeanza kazi.
Hivi kwa mtindo huu tunategemea maandamano yapungue au kuisha? Maisha yapo juu na mfumuko wa bei umekuwa juu sambamba na kushuka kwa thamani ya shilingi, tulitegemea Rais angetoa tamko la jinsi ya kudhibiti haya yote ila imekuwa kinyume kabisa.
Wananchi inapaswa tuamke sasa na tuchukue hatua, hivi palikuwa na haja gani ya kutumia mamilioni yote hayo kusherekea miaka 50 ya Uhuru? Inamnufaisha nini mwananchi wa kawaida? Miaka 50 ya uhuru ni kwa ajili ya viongozi wanaojiongezea mishahara kila wanapojisikia na ingekuwa heri kama wananchi wangezisusia sherehe hizi za kinafki.
Nchi imeshika nafasi ya tatu kwa kupewa misaada duniani na ya kwanza Afrika, nafasi ya juu kwa rushwa na miongoni mwa nchi 50 maskini zaidi duniani. Kwa mtindo huu kazima tulazimishwe kuukubali ushoga ili tupewe misaada. Tafakari, chukua hatua.....

No comments:

Post a Comment