Kutokana na mvua kubwa zinazoambatana na Radi zinazoendelea katika jiji la Dar es salaam toka mishale ya saa 10 alfajiri, zimesababisha kukatika kwa umeme katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nguzo za umeme zimedondoka kama eneo la Ubungo na Tabata Segerea jambo ambalo limeilazimu Tanesco kuzima umeme baadhi ya maeneo kuepusha hatari.
Nikizungumza na moja ya wafanyakazi wa kitengo cha mawasiliano asubuhi hii ambae hakuwa tayari jina lake kuwekwa hapa amesema wananchi wanapaswa kutembea kwa makini wakati huu wa mvua na endapo utaona popote ambapo nguzo imedondoka au nyaya kukatika na matatizo mengine ya umeme toa taarifa Tanesco mara moja, ameendelea kusema katizo hili la umeme ni la muda na hali itakapokuwa shwari watashughulikia baadhi ya maeneo yenye matatizo na shughuli zitaendelea kama kawaida.
Tanesco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
VIONGOZI WA CCM KATIKA PICHA Z’BAR
9 hours ago
No comments:
Post a Comment