Jana majira ya saa 6:30 mchana katika chuo kikuu mlimani palitokea aibu kubwa ambayo itabaki kumbukumbu. Wanafunzi wa UDSM waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya kuwapokea Marais wawili waliokuwa wageni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 ya kitivo cha sheria chuoni hapo ambao wote ni wahitimu chuoni hapo kwa nyakati tofauti walikumbwa na aibu hiyo.
Mwenyeji wa shughuli hiyo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya muungano Mh. J.M. Kikwete akiongozana na mgeni mwalikwa ambae ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa na Rais Mstaafu Mzee AlHassan Mwinyi waliingia chuoni hapo mishale ya saa 6 mchana na mara tu baada ya kufika ndipo walipokumbwa na zomeazomea hiyo huku wanafunzi hao wakiimba ' Kama sio juhudi zako Nyerere x 3 mafisadi wangesoma wapi?'.
Naunga mkono swala hilo huku nikianza kukosoa matatizo mbalimbali ambayo serikali inayoongozwa na J.K imeshindwa kuyatatua huku mara nyingi akilalamikia watendaji wake kumkwaza, swali ni je amechukua hatua gani? Hebu jiulize alitegemea kushangiliwa na wanachuo hao kwa lipi? Kama ameshindwa kushughulikia matatizo mbalimbali yanayolikumba Taifa atashangiliwa kwa lipi?
Unawezaje kumshangilia Rais huku unakufa kwa njaa kutokana na mfumuko wa bei na kushuka kwa shilingi? Utamshangiliaje Rais huku Nishati muhimu kwa maendeleo(Umeme) umekuwa haueleweki huku yeye akicheka na wahusika? Unamshangiliaje Rais huku mikopo kwa wanavyuo ikiwa haieleweki na idadi kubwa ya wanaostahili hawapati? Huku baadhi ya vyuo kama Tumaini Dar es Salaam College kikiendelea kutoza ada kubwa mno (2.4million per year) na huduma zikiwa ni mbovu mno, wanafunzi wanasomea chini ya miti, maktaba ikiwa haina vitabu vya kutosha na matatizo ya uhaba wa wakufunzi. Wengi hawapendi kwenda pale ila wanajikuta tayari wamepangwa na bodi ya vyuo TCU Je Rais alitegemea kushangiliwa na watu wenye machungu kama hawa?
Lazima ufike wakati watanzania tuache unafiki na tumpatie kila mtu kile anachostahili, kwa lipi kati ya hayo lingemfanya ashangiliwe? Huku wanafunzi wakishindwa kulipa malipo ya hosteli kutokana na kuchelewa kwa mikopo na wakikabwa koo na mama ntilie mtaani, wana lipi la kufurahia? Nadhani hilo ni funzo tosha na kama mabadiliko yasipofanywa ategemee fedheha kubwa zaidi toka kwa wasomi ambao wanaelewa matatizo chungu nzima ya nchi hii yanayotokana na utawala mbovu.
Unawezaje kuwalipa Dowans 94bn huku Mtanzania wa kawaida akiumia na makali ya maisha kwa uzembe wa watu wawili au watatu walioingia mikataba dhalimu na ya kifisadi? Wanajulikana ila Rais amechukua hatua gani? Ifike wakati tuseme basi, nawapongeza UDSM kwa ujasiri wao na wamefungua njia.
Tuamke Watanzania
WELCOME
MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED
BE BLESSED
MY DIARY

- RONALDTHEGREAT
- Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
- FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE
RONNIE DOCOMENTARY
-
▼
2011
(157)
-
▼
October
(18)
- MAKALI YA MGAO WA UMEME KUREJEA UPYA: WAZIRI WA FE...
- ZITTO AHAMISHIWA ICU:ANA VIJIDUDU 150 VYA MALARIA,...
- BASI LA SUMMRY TOKA DAR-DOM LAPATA AJALI MBAYA, JI...
- WATATU WAFA KWA KIPIGO CHA POLISI DODOMA: NANI ANA...
- NANI ANAWAPA POLISI NGUVU YA KUPIGA RAIA NA KUHARI...
- KILICHOMTOKEA JK UDSM NI HALALI KABISA:NCHI INANUKA
- GHADDAFI ADAIWA KUKAMATWA NA MAJESHI YA NATO
- SHAME: JK AZOMEWA NA WANAFUNZI WA UDSM
- MTANGAZAJI AJITANGAZA SHOGA KWENYE TAARIFA YA HABARI
- USHAURI WA BURE KWA SERIKALI
- MITAMBO MIPYA YA AGGRECO YAPATA HITILAFU KUBWA
- LETS FIGHT AGAINST MALARIA: Miss Mtwara 2011/12 af...
- KADA WA CCM ATAMANI UPINZANI USHINDE MWAKA 2015: A...
- CHRISS BROWN ANG'AA KATIKA BET 2011 AWARDS
- MSHINDI WA BSS APATIKANA
- TUTAFIKA KWELI KWA KAULI ZA VIONGOZI? - Dr H.K Kin...
- CCM WASHINDA KWA TABU iGUNGA Chama Cha Mapind...
- http://www.mwananchi.co.tz/
-
▼
October
(18)
Popular Posts
-
12 World’s weirdest stadiums A lot of stadiums around the world have spectacular designs, like the new World Cup 2010 stadiums in South A...
-
Usajili uliokamilika kwa timu za Uingereza Everton -Nikica Jelavic toka Rangers Tottenham - Louis Saha toka Everton QPR - Djibril Cis...
-
Pink Hummer Limo Three TVs, laser lights , strobes, 1800 watt sound system, Disco Floor, star lights, optic lights, pink leather interior, ...
-
INTERNATIONAL WOMEN’S DAY CENTENARY CELEBRATIONS: 1911-2011 DECENT WORK, DECENT LIVES: 100 YEARS OF HERSTORY CONCEPT NOTE Synopsis The 8...
-
Tanzania kwa mara ya kwanza tumepata bahati ya moja ya vivutio vyetu vya Utalii na moja ya lebo ya Taifa mlima Kilimanjaro kutajwa kuingia k...
-
PRESIDENT Jakaya Kikwete has warned the opposition PRESIDENT Jakaya Kikwete has warned the opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo...
-
Timu ya Liverpool na Manchester City zimeonja chungu ya kufungwa ugenini baada ya kupoteza michezo yake ya Europa League hapo jana. Liverp...
-
Haya ndiyo baadhi ya yaliyoamuliwa kuhusu madai ya Madaktari Kwa ufupi, kutoka kwa watu waliokuwemo kwenye mkutano wa Madaktari na Waziri Mk...
-
Miss Mtwara mwaka 2011/12 Rahma Swai amefariki dunia kwa Ugonjwa wa malaria, mlimwende huyo ambae alikuwa moja ya washiriki wa Shindano la V...
-
The boy octopus An eight-Deepak Kumar from India became a normal child after his parasitic twin was removed by surgery. In India, the b...
OTHER BLOG LIST
Thursday, October 20, 2011
KILICHOMTOKEA JK UDSM NI HALALI KABISA:NCHI INANUKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment