WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Saturday, October 22, 2011

WATATU WAFA KWA KIPIGO CHA POLISI DODOMA: NANI ANAWAPA HAWA POLISI NGUVU HII?

"Tanzania hakuna amani"x 4 ni kilio kilichoonekana ka,a wimbo nilichokisikia nikiwa nimetegea sikio taarifa ya habari katika stesheni fulani maarufu hapa nchini usiku wa leo, nimepatwa na mshtuko mkubwa ulionifanya nikae chini na kuandaa makala hii. Ni kilio toka kwa wananchi toka Dodoma, makao makuu ya nchi waliokuwa wakipokea kipigo toka kwa askari polisi wakifukuzwa kumpisha mwekezaji katika eneo alilouziwa.
Matukio ya polisi kupiga Raia katika utawala huu wa awamu ya nne yamekuwa ni gumzo lisilomalizika, maeneo ,mbalimbali hapa nchini matukio haya yamekuwa ni wimbo usiomalizika pasina hatua yoyote madhubuti inayochukuliwa na serikali hii dhaifu.
Hebu jiulize hao wawekezaji toka nje wanaouziwa maeneo waliyoyatunza mababu zetu na kuturithisha, na watanzania wazalendo wapi wenye haki? isitoshe wawekezaji wenyewe wanapopewa hayo maeneo huishia kuyatumia kwa manufaa yao huku wananchi wa kandokando inapopatikana miradi hiyo wakiachwa katika hali ngumu. Hakuna shule, hakuna maji na huduma nyingine muhimu, mwekezaji huyu ana faida gani?
Swali kubwa lililobaki kichwani mwangu ni au kwakuwa maeneo yale wanakaa fukara? Mbona kuna viongozi wanamiliki maelfu ya hekari na hatusikii migogoro ya ardhi yao na wawekezaji? Hao polisi waliopiga wananchi huko Dodoma na kuharibu mali zao wanapewa nguvu na nani? Unadhani ni pesa kiasi gani inatosha kumhamisha mtu katika eneo alilokaa zaidi ya miaka 20? Hivi hao wanaokadiria tjamani ya nyumba na mali zilizomo wanadhani hiki ni kipimo tosha?
Nawaza mengi na sidhani kama Mwalimu Nyerere angerudi angevumilia mateso haya wanayopata watanzania, kweli kwa hali kama hii unategemea wananchi kumshangilia kiongozi wa nchi? Kwa lipi? Mkuu wa mkoa na wa Wilaya walikuwa wapi wakati wananchi wale wakidhalilishwa? Wanafanya kazi gani viongozi hawa wa kisiasa wanaolindwa na mwavuli wa serikali? Nimefurahia Zambia kuondolewa kwa vyeo hivi visivyo na msingi ambapo nchini hapa wanapewa wale walioshindwa ubunge maeneo yao au kukosa uwaziri ili waendelee kula, wale walioenda shule wayakuwa wanauona mfumo huu maarufu kama "Klepocracy"
Wakati baba na mama wakiadhibiwa mbele ya watoto wao na Polisi waliotumwa na serikalu walioichagua huku wakiimba hadi makoo kukauka katika kampeni, viongozi hawa wametulia majumbani mwao wakipanga nchi ya kwenda kutembea kwa madai ya kutafuta uwekezaji. Huyu mwekezaji anasababisha udhalilishaji huu ametoka mbinguni? Nimesikitishwa na mwanamama aliyekuwa akilia kilio kikuu huku akitamka "Tanzania hakuna amani" x 4.
Huu ni wakati muafaka kwa wananchi kuamua wenyewe na kujionea serikali wanazozichagua na kazi wanayofanya, watanzania wanabebeshwa mizigo mizito na watu wachache wasiotambua shida ni nini, wao wakiumwa mafua tu kutibiwa Ujerumani huku wakisaini mikataba dhalimu inayowanufaisha wao na familia zao huku walalahoi wakiachwa wakiwa hawana la kufanya na kupata fedheha kama hii.
Naitazama amani yetu kwa jicho la tatu, aidha yataibuka mapigano kati ya sisi na hao wawekezaji au kati ya sisi wananchi na viongozi hawa wazembe wanaouza rasilimali zetu kila kukicha kwa kivuli cha uwekezaji. Hivi Moreno Ocampo hayaoni haya? NATO na UN hawaoni udhalilishaji huu? Mkataba wa haki za binadamu wa mwaka 1948 tuliosaini ndio unatuongoza hivi? Uko wapi umuhimu wa kuwa na makamu katibu wa UN?
Poleni sana wananchi ,mliodhalilishwa na kuonekana kama wakimbizi katika nchi yenu, mungu anasikia kilio chenu. Na huu ndio wakati muafaka kwenu kufungua macho na kufanya maamuzi sahihi 2015.

No comments:

Post a Comment