WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Thursday, October 20, 2011

SHAME: JK AZOMEWA NA WANAFUNZI WA UDSM

Huku hali ikiendelea kuwa tete kwa Chama Cha Mapinduzi sambamba na viongozi wake ambapo wanatafunwa na siasa za makundi, baadhi ya matukio yamekuwa yakiibuka ambapo yanawaacha watu midomo wazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya M. Kikwete amezomewa na wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam alipodhuru chuini hapo kwa kushindwa kushughulikia matatizo mbalimbali yanayowakumba wanavyuo mbalimbali nchini ikiwamo swala la mikopo sambamba na matatizo mbalumbali yanayoikumba nchi ikiwamo kushuka kwa thamani ya shilingi sambamba na kupanda kwa gharama za maisha na matatizo mengineyo likiwamo la umeme
Mambo yakiwa hayajatulia ndani ya Chama baada ya fukuto la uchaguzi wa Igunga ambapo CCM walishinda kwa tabu japo jimbo lilikuwa mikononi mwao toka mwaka 1994 chini ya Rostam Aziz, tukio jingine lililowashangaza watu ni fujo zilizoikumba UVCCM huko Arusha sambamba na kujisafisha katika vyombo vya habari kwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa huku akitishia atawashtaki wote watakaotumia jina lake vibaya katika vyombo vya habari.
Mmmmmmh hali ni mbaya kwa kweli, hii ni Tanzania tunayoitaka?

1 comment:

  1. Kimya kingi kina mshindo mkuu.....Siku yatakapolipuka yaliyojaa kwenye mioyo ya watanzania wengi ambao ni masikini....Ndipo watakapofunguka mafisadi hawa wanaojilimbikizia mali... Na hawa viongozi ambao hawawezi kuchukua hatua yeyote kwa kuwa nao wametekwa kimaslahi....

    ReplyDelete