"Tanzania hakuna amani"x 4 ni kilio kilichoonekana ka,a wimbo nilichokisikia nikiwa nimetegea sikio taarifa ya habari katika stesheni fulani maarufu hapa nchini usiku wa leo, nimepatwa na mshtuko mkubwa ulionifanya nikae chini na kuandaa makala hii. Ni kilio toka kwa wananchi toka Dodoma, makao makuu ya nchi waliokuwa wakipokea kipigo toka kwa askari polisi wakifukuzwa kumpisha mwekezaji katika eneo alilouziwa.
Matukio ya polisi kupiga Raia katika utawala huu wa awamu ya nne yamekuwa ni gumzo lisilomalizika, maeneo ,mbalimbali hapa nchini matukio haya yamekuwa ni wimbo usiomalizika pasina hatua yoyote madhubuti inayochukuliwa na serikali hii dhaifu.
Hebu jiulize hao wawekezaji toka nje wanaouziwa maeneo waliyoyatunza mababu zetu na kuturithisha, na watanzania wazalendo wapi wenye haki? isitoshe wawekezaji wenyewe wanapopewa hayo maeneo huishia kuyatumia kwa manufaa yao huku wananchi wa kandokando inapopatikana miradi hiyo wakiachwa katika hali ngumu. Hakuna shule, hakuna maji na huduma nyingine muhimu, mwekezaji huyu ana faida gani?
Swali kubwa lililobaki kichwani mwangu ni au kwakuwa maeneo yale wanakaa fukara? Mbona kuna viongozi wanamiliki maelfu ya hekari na hatusikii migogoro ya ardhi yao na wawekezaji? Hao polisi waliopiga wananchi huko Dodoma na kuharibu mali zao wanapewa nguvu na nani? Unadhani ni pesa kiasi gani inatosha kumhamisha mtu katika eneo alilokaa zaidi ya miaka 20? Hivi hao wanaokadiria tjamani ya nyumba na mali zilizomo wanadhani hiki ni kipimo tosha?
Nawaza mengi na sidhani kama Mwalimu Nyerere angerudi angevumilia mateso haya wanayopata watanzania, kweli kwa hali kama hii unategemea wananchi kumshangilia kiongozi wa nchi? Kwa lipi? Mkuu wa mkoa na wa Wilaya walikuwa wapi wakati wananchi wale wakidhalilishwa? Wanafanya kazi gani viongozi hawa wa kisiasa wanaolindwa na mwavuli wa serikali? Nimefurahia Zambia kuondolewa kwa vyeo hivi visivyo na msingi ambapo nchini hapa wanapewa wale walioshindwa ubunge maeneo yao au kukosa uwaziri ili waendelee kula, wale walioenda shule wayakuwa wanauona mfumo huu maarufu kama "Klepocracy"
Wakati baba na mama wakiadhibiwa mbele ya watoto wao na Polisi waliotumwa na serikalu walioichagua huku wakiimba hadi makoo kukauka katika kampeni, viongozi hawa wametulia majumbani mwao wakipanga nchi ya kwenda kutembea kwa madai ya kutafuta uwekezaji. Huyu mwekezaji anasababisha udhalilishaji huu ametoka mbinguni? Nimesikitishwa na mwanamama aliyekuwa akilia kilio kikuu huku akitamka "Tanzania hakuna amani" x 4.
Huu ni wakati muafaka kwa wananchi kuamua wenyewe na kujionea serikali wanazozichagua na kazi wanayofanya, watanzania wanabebeshwa mizigo mizito na watu wachache wasiotambua shida ni nini, wao wakiumwa mafua tu kutibiwa Ujerumani huku wakisaini mikataba dhalimu inayowanufaisha wao na familia zao huku walalahoi wakiachwa wakiwa hawana la kufanya na kupata fedheha kama hii.
Naitazama amani yetu kwa jicho la tatu, aidha yataibuka mapigano kati ya sisi na hao wawekezaji au kati ya sisi wananchi na viongozi hawa wazembe wanaouza rasilimali zetu kila kukicha kwa kivuli cha uwekezaji. Hivi Moreno Ocampo hayaoni haya? NATO na UN hawaoni udhalilishaji huu? Mkataba wa haki za binadamu wa mwaka 1948 tuliosaini ndio unatuongoza hivi? Uko wapi umuhimu wa kuwa na makamu katibu wa UN?
Poleni sana wananchi ,mliodhalilishwa na kuonekana kama wakimbizi katika nchi yenu, mungu anasikia kilio chenu. Na huu ndio wakati muafaka kwenu kufungua macho na kufanya maamuzi sahihi 2015.
WELCOME
MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED
BE BLESSED
MY DIARY
- RONALDTHEGREAT
- Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
- FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE
RONNIE DOCOMENTARY
-
▼
2011
(157)
-
▼
October
(18)
- MAKALI YA MGAO WA UMEME KUREJEA UPYA: WAZIRI WA FE...
- ZITTO AHAMISHIWA ICU:ANA VIJIDUDU 150 VYA MALARIA,...
- BASI LA SUMMRY TOKA DAR-DOM LAPATA AJALI MBAYA, JI...
- WATATU WAFA KWA KIPIGO CHA POLISI DODOMA: NANI ANA...
- NANI ANAWAPA POLISI NGUVU YA KUPIGA RAIA NA KUHARI...
- KILICHOMTOKEA JK UDSM NI HALALI KABISA:NCHI INANUKA
- GHADDAFI ADAIWA KUKAMATWA NA MAJESHI YA NATO
- SHAME: JK AZOMEWA NA WANAFUNZI WA UDSM
- MTANGAZAJI AJITANGAZA SHOGA KWENYE TAARIFA YA HABARI
- USHAURI WA BURE KWA SERIKALI
- MITAMBO MIPYA YA AGGRECO YAPATA HITILAFU KUBWA
- LETS FIGHT AGAINST MALARIA: Miss Mtwara 2011/12 af...
- KADA WA CCM ATAMANI UPINZANI USHINDE MWAKA 2015: A...
- CHRISS BROWN ANG'AA KATIKA BET 2011 AWARDS
- MSHINDI WA BSS APATIKANA
- TUTAFIKA KWELI KWA KAULI ZA VIONGOZI? - Dr H.K Kin...
- CCM WASHINDA KWA TABU iGUNGA Chama Cha Mapind...
- http://www.mwananchi.co.tz/
-
▼
October
(18)
Popular Posts
-
Whitney Houston, who reigned as pop music's queen until her majestic voice and regal image were ravaged by drug use, erratic behavior an...
-
MR II G SOLO ANTI VIRUS PART 1 COVER SOGGY DOGGY ZAY B SUMA G Picha za juu hapo ni baadhi ya wasanii watakaotumbuiza...
-
If you want to know how to your ex back and don’t know where to start, follow this simple step-by-step action plan to get your ex back. I...
-
AUSAMBAZA KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKE WA KARIBU NAIBU Waziri wa Ujenzi anayeugua ugonjwa uliozusha utata mkubwa serikalini, Dk. Harris...
-
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameendelea kusisitiza kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harriso...
-
The Football Association have confirmed that Fabio Capello has resigned as England manager. The Italian tendered his resignation following a...
-
How To Be Creative by ronald Do you ever get asked ‘Where did you get that idea from?’ in any of your projects or pieces of work and yo...
-
Carlos Tevez has been told he must make grovelling apologies before pulling on a Manchester City shirt again. THE SUN Arsene Wenger has ad...
-
Timu za soka zinazotokea katika jiji la London na zilizo katika Big 4 ya ligi kuu ya England zimewaonya mashabiki wake kujiepusha na vitendo...
-
UTAFITI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini ni wagumba ukipingana madai ya wengi kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake.Kwa muji...
OTHER BLOG LIST
Saturday, October 22, 2011
NANI ANAWAPA POLISI NGUVU YA KUPIGA RAIA NA KUHARIBU MALi ZAO? MIAKA 50 YA UHURU HAIMFAIDISHI MLALAHOI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment