WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

Popular Posts

Thursday, October 20, 2011

MTANGAZAJI AJITANGAZA SHOGA KWENYE TAARIFA YA HABARI

Mtangazaji wa televisheni ya ABC nchini Marekani Danny Cliff amejitangaza kuwa yeye ni shoga katika taarifa ya habari ya kituo hicho ambapo yeye ndie alikuwa msomaji.
Hali hiyo ya kushangaza iliwaacha wengi vinywa wazi kwani ni jambo ambalo hawakulitegemea, Danny ambae swala la yeye kuwa shoga lilikuwa likifahamika na ndugu na marafiki wa karibu amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kinyanyasaji vinavyowakumba baadhi ya mashoga duniani kote na akitolea mfano wa mwanafunzi mwenye miaka 14 aliyejiua huko Marekani baada ya wanafunzi wenzie kuwa wanamwandama na kumnyanyasa baada ya kujitangaza hadharani kuwa ni shoga.
Hivi karibuni ambapo shoga mmoja aliomba haki zao kutambuliwa katika jamii na katiba mpya iwafikirie kama sehemu ya jamii katika kongamano la jinsia lililoandaliwa na TGNP na pia shoga mwingine maarufu hapa nchini maarufu kama Aunt Suzy alijitangaza hadharani katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm ambapo pia baada ya hapo alipata shambulio toka kwa mwanaume aliyekuwa anaishi nae.
Tutafika kweli? Hii inaashiria nini? Je tuwatambue hawa kama moja ya wanajamii?

1 comment:

  1. Tatizo binadamu tunapenda sana kuhukumu... aliyemuumba hajamua kumtengenezea dunia yake peke yake wala kumtenga, ila wewe kwa ubinafsi wako kisa tu hajaumbwa kama wewe basi utataka umtenge na kumyanyasa...si kazi yetu kuhukumu kwa sababu na sisi tunamapungufu yetu makubwa zaidi kuliko wao na hakuna anayetutenga.
    Mbona sioni wanaume wakiwanyanyapaa na kuwatenga wasichana waliotoa mimba...hilo si kosa la mauaji? Si amepunguza nguvukazi ya taifa? Huyo kwa ushoga wake, kamdhuru nani? Si bado anajenga taifa- anafanya kazi, analipa kodi, na nanaishi kama watu wengine ila tofauti ni kuwa hapendi wanawake kimapenzi bali wanaume?! Ulipokuwa hufahamu ni shoga alikudhuru nini...ila kufahamu tu kuwa ni shoga ghafla kawa mtu mbaya sana?! Tunapoteza muda mwingi sana katika mawazo hasi kuliko chanya!

    ReplyDelete