Majambazi yaliyokuwa na silaha nzito yamevamia katika kituo cha mafuta cha TOTAL kilichopembeni ya Mlimani City Supermarket na kupora mamilioni ya pesa.
Tukio hilo limetokea mishale ya saa6 - 7 ambapo majambazi hao wakiwa na silaha nzito walifunga eneo hilo kwa milio ya risasi na kupora kiasi kikubwa cha pesa ambacho hakijathibitishwa hadi sasa na kutoweka nazo kusikoeleweka. Polisi imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini majambazi hao ambapo mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya mtu aliyejeruhiwa au kupoteza maisha katika tukio hilo.
Matukio ya ujambazi yameendelea kulitikisa jiji la Dar es Salaam huku njia sahihi ya kukabiliana nao ikiwa bado haijavumbuliwa na mara nyingi Polisi wakionekana kuzidiwa nguvu na ujanja na majambazi ambao mara nyingi huwa na silaha nzito.
Habari zaidi baadae
HABARI NJEMA KWA WAFUGAJI
15 hours ago
lini?
ReplyDelete