UTANGULIZI
Mgomo wa Madaktari ambao umedumu kwa takriban wiki mbili nchini sasa ni dhahiri kwamba umelitikisa Taifa na kuathiri huduma za tiba katika hosipitali kadhaa nchini. Mgomo huu ulianza taratibu na kuendelea kukua kutokana na mvutano, pia vita ya maneno baina ya Serikali na Madaktari. HALI ILIVYO SASA Kutokana na taarifa zinazofikishwa katika vyumba vya habari, ni dhahiri kwamba hali ni mbaya sana katika baadhi ya hosipitali nchini hasa Hosipitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo mgomo huu umesababisha vifo vya watu ambao huenda wangepona kama wangepata huduma. Wagonjwa mahututi wanaofikishwa MNH kwa ajili ya huduma za rufaa hawapokelew,maiti wanaofikishwa kwa ajili ya kuhifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary), hawapewi hifadhi na badala yake wanarejeshwa walikotoka. Hata katika hosipitali ambazo madaktari wameripotiwa kurejea kazini, huduma zinazotolewa ni hafifu hii ikimaanisha kwamba mgomo bado unaendelea hata kama si kwa madaktari kukutana kwenye kumbi kama ilivyokuwa mwanzo. Madaktari kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamepelekwa katika hosipitali za Serikali kuokoa jahazi, hawatoshelezi lakini katika baadhi ya maeneo wamepata upinzani kutoka kwa wauguzi wa hosipitali husika. MAPENDEKEZO Kutokana na hali ilivyo sasa, Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika kikao cha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kilichokutana leo Jumanne 31 Januari 2012, wamesema “Inatosha” kwa na kwamba hali isiachwe ikaendelea na kupendekeza yafuatayo: Pande husika katika mgogoro huu ambazo ni Serikali na Madaktari wakubali kukaa katika meza moja ya mazungumzo kutafuta mwafaka wa suala hili, wenye lengo la kupata suluhu ya tatizo lililopo, huku kila upande ukiangalia madhara kwa binadamu yanayotokana na mgogoro huu. Majadiliano yalenge kutatua matatizo ya madaktari kwa upande mmoja, lakini pia yazingatie uwezo wa Serikali kwa upande mwingine. Nia iwe ni kuwawezesha madaktari kadri uwezo wa Serikali unavyoruhusu lakini pia kuwaokoa wagonjwa ambao wanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na kukosa tiba. Madaktari wakubali kurejea kazini haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya watu ambao wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma za tiba, wakati wagonjwa wakiwa si sehemu ya mgogoro uliopo. Serikali ifute amri zake zote dhidi ya madaktari waliokuwa kwenye mgomo (hasa ile ya kuwafukuza wasiofika kazini jana Jumatatu Januari 30, 2012) ili kuwezesha mazungumzo kufanyika baina ya pande hizo mbili. Baada ya makubaliano kufikiwa, iwepo kalenda ya utekelezaji wa makubaliano husika ili kuepusha kutokea kwa mgomo mwingine ambao unaweza kuleta athari kubwa zaidi kwa wananchi. Baada ya maafikiano kuwapo, usiwepo mpango wowote wa wazi au wa kificho wa kuwaadhibu kwa namna yoyote ile viongozi wa madaktari waliogoma kwani tunaamini kwamba madai yao yalikuwa halali. Serikali kuanzia sasa ifanye mapitio ya mishahara, maslahi na stahili nyingine za wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na kuyaboresha, ili kuepuka kufanya hivyo kwa shinikizo la migomo inayofanywa na watumishi hao kwa makundi. HITIMISHO Wakati tukiamini kwamba busara itatumika kuliondoa Taifa letu katika mtanziko uliopo, tuseme wazi kuwa sisi Wahariri tunaamini yafuatayo: Kwanza tunatambua umuhimu wa kada ya udaktari kwa umma, hivyo kutambua haki yao ya kupata mahitaji muhimu. Ikiwa madaktari hawapati mahitaji muhimu, basi ni dhahiri kwamba hawawezi kutoa huduma kwa wagonjwa ipasavyo. Pili tunatambua pia ufinyu wa rasilimali za nchi ambazo pengine ndicho kikwazo kwa Serikali kushindwa kuwalipa watumishi wake vizuri au kadri ya madai yao, licha ya kwamba wawakilishi kama wabunge wamepewa nyongeza ya posho za vikao kwa viwango ambavyo vimezua manung'uniko kutoka kwa umma. Lakini tofauti zozote zilizopo, ziwe za kiutendaji au kiutawala kamwe haziwezi kuondolewa bila pande husika kukubali kukaa na kuzijadili ili kupata mwafaka kwa faida ya Watanzani wote. Ni matumaini yetu kwamba busara zitatumika ili kuwaokoa Watanzania. Neville Meena KATIBU WA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF
WELCOME
MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED
BE BLESSED
MY DIARY
- RONALDTHEGREAT
- Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
- FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE
RONNIE DOCOMENTARY
-
▼
2012
(43)
-
▼
February
(35)
- MANDELA IN "SATISFACTORY CONDITION" AFTER OPERATION
- ARSHAVIN, SAMBA WAKIMBILIA RUSSIA
- ARSENAL & TOTTENHAM ZAONYA MASHABIKI WAKE
- WARAKA WA SIRI TOKA KWA MH. HARRISON MWAKYEMBE
- SUGU NA RUGE WAPATANISHWA
- SITTA - MWAKYEMBE KALISHWA SUMU, POLISI WANAPOTOSHA
- WIZARA YA AFYA YAMRUKA DCI MANUMBA:NI KUHUSU TAARI...
- ASAMOAH GYAN QUITS INTERNATIONAL FOOTBALL
- TAARIFA YA DKT HARRISON MWAKYEMBE KUJIBU KAULI YA ...
- WENGER TO SELL WALCOTT & OTHER 5 PLAYERS IN SUMMER...
- MAJAMBAZI YAVAMIA ENEO LA MLIMANI CITY
- MATOKEO YA MICHEZO YOTE YA EUROPA ILIYOFANYIKA JAN...
- HABARI ZILIZOPAMBA MAGAZETI YA SOKA ULAYA LEO
- HONDURAS: FIRE KILLS 300 PRISONERS IN JAIL
- KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED KITAKACHOIVAA AJAX KA...
- HABARI ZILIZOPEWA KIPAUMBELE MAGAZETI YA SOKA ULAY...
- ARSENAL KUVAA JEZI TOFAUTI LEO DHIDI YA AC MILAN
- BARCA, LYON ZAANZA VIZURI 16 BORA UEFA
- FA TO PUNISH SUAREZ
- R.I.P: WHITNEY HOUSTON 48 DIED
- WONDERFUL: PROSTITUTES IN LUSAKA OFFER FREE SEX FO...
- TAARIFA TOKA TANESCO JUU YA MGAO UNAOENDELEA
- YALIYOAMULIWA KUHUSU MADAI YA MADAKTARI:MASHARTI W...
- The list is compiled by gathering income streams f...
- MCHANGANUO WA MATOKEO KIDATO CHA NNE: DARAJA LA KW...
- WACHORA PICHA, KUANDIKA MATUSI NA VERSE ZA BONGO F...
- FABIO CAPELLO RESIGNED TO COACH ENGLAND
- UTAFITI: NUSU YA WANAUME NCHINI NI WAGUMBA
- TAARIFA MAALUM KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TOKA JUKW...
- KAULI NA MSIMAMO WA MBUNGE jOHN MNYIKA KUHUSU MGOM...
- MADAKTARI BINGWA MUHIMBILI WAGOMA RASMI
- BARIDI INAYOENDELEA ULAYA YAUA 300
- YASEMAVYO MAGAZETI YA SOKA ULAYA LEO.
- TERRY APOKONYWA UNAHODHA ENGLAND
- MASHABIKI 74 WAFARIKI KATIKA FUJO MISRI
-
▼
February
(35)
Popular Posts
-
A massive fire has swept through a jail in Honduras, killing at least 300 prisoners, officials say. Many victims were burned or suffocated t...
-
The 5,000 sq ft home includes a saltwater pool, glassed in sunroom, outside fireplace, 5 bedrooms and 5 baths ... but no apparent grotto,...
-
PFA chief executive Gordon Taylor believes it is time for the FA to intervene after Luis Suarez and Patrice Evra failed to shake hands befor...
OTHER BLOG LIST
Tuesday, February 7, 2012
TAARIFA MAALUM KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TOKA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA(TEF)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment