WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Wednesday, February 8, 2012

WACHORA PICHA, KUANDIKA MATUSI NA VERSE ZA BONGO FLEVA KATIKA KARATASI ZA MAJIBU KIDATO CHA NNE 2011

Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaoonesha kuwa asilimia 53.59 ya wanafunzi 426,314 waliofanya mtihani huo wamefaulu. Hata hivyo, wakati asilimia hiyo ambayo ni sawa na wanafunzi 180,216 wakifurahia matokeo hayo, wenzao 3,301 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu ikiwamo mfanano usio wa kawaida wa majibu. Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Joyce Ndalichako alisema, NECTA imefuta matokeo ya watahiniwa 3,03 waliobainika kufanya udanganyifu kati yao, watahiniwa wa shule ni 3,301 na wawili wakiwa wa maarifa (QT). Watahiniwa 182 walikamatwa na wasimamizi wakiwa na makaratasi (notes) sita walikamatwa na simu, watatu walikuwa wakifanyiwa mtihani na watu wengine, wanne walisajiliwa kufanya mtihani kwa majina ya watu wengine. Watahiniwa 2,896 karatasi zao za majibu zilikuwa na mfanano usio wa kawaida, 155 karatasi zao za majibu zilikuwa na miandiko zaidi ya mmoja, 14 kubadilishana karatasi katika chumba cha mtihani, 18 kukamatwa na karatasi za majibu zaidi ya moja, 25 wakiwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu, kuwa na vikaratasi ama kubadilishana vikaratasi. “Mtu mmoja unakuta mitihani yake ya majibu ina miandiko zaidi ya 10, na jeshi la polisi ndilo lililothibitisha kuwa miandiko ya wanafunzi hawa ilikuwa inatofautiana. Baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa nane walioandika matusi ya nguoni kwenye karatasi zao za majibu. “Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu kinaonyesha utovu wa nidhamu, hivyo pamoja na kuwafutia matokeo ufuatiliaji zaidi unaendelea ili kuona hatua za kuwachukulia,” alisema Dkt. Ndalichako. Pia alitoa onyo kali kwa vituo vilivyohusika na udanganyifu huo, huku akisema kwa vilivyobaika vitaandikiwa barua ya kutaka vijieleze kwa nini visifutiwe matokeo. Akasema baadhi ya watahiniwa waliandika nyimbo za kizazi kipya (Bongo fleva) kwenye karatasi zao za majibu huku wengine wakichora michoro isiyo eleweka na wachezaji wa mpira. “Mwingine aliandika bongo fleva, ngoja niwasomee, wasahihishaji msinisamehe..., ,"ACHA UTANI NA GIRLI WANGU.... NAKUJA HOME NAKUKUTA...... NIKIFELI MTIHANI NAENDELEA NA FANI YA MUZIKI" Dkt. Ndalichako alisoma moja ya karatasi za majibu za watahiniwa hao huku akiruka baadhi ya maeneo akisema ameandika matusi yasiyoweza kusomeka. (gazeti la Mwananchi

No comments:

Post a Comment