WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Tuesday, March 8, 2011

BARCA Vs ARSENAL NI BALAA TUPU

AMA ZAO, AMA ZETU:Arsenal na Barcelona hakuna kulala

Mshambuliaji wa Barca
MADRID, HISPANIA
KUKOSEKANA kwa Robin van Persie na Theo Walcott katika kikosi cha Arsenal kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Barcelona, leo Jumanne kunamaanisha kuwa timu hiyo ya London itatakiwa kujihami zaidi kuliko kushambulia.

Kikosi cha Arsene Wenger kilionyesha soka la hali ya juu wakati kiliposhinda kwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo na kitatakiwa kujizatiti zaidi katika mechi ya marudiano ili kupiga hatua.

Katika mechi hiyo Van Persie na Andrei Arshavin ndio waliopachika mabao ya ushindi.

Lakini tangu wakati huo, Arsenal imepita katika wakati mgumu ambapo walipoteza mechi ya fainali ya Kombe la Carling mbele ya Birmingham City.

Timu hiyo ilikuwa ikiikimbiza vema Manchester United kwenye ubingwa wa Ligi Kuu England, lakini ilikavutwa shati na Sunderland Jumamosi wakati zilipotoka suluhu.

Wenger alikasirika kwa kuwa timu yake ilishindwa kuifunga Sunderland na hasira zake ziliongezeka maradufu baada ya Jack Wilshere kuumia.

Lakini Cesc Fabregas aliyekosa mechi dhidi ya Sunderland ataingia uwanjani kupambana na Barcelona.

Na kwa kuwa Walcott na Van Persie hawatakuwepo, Wenger anafahamu mbinu pekee ni kutengeneza ukuta.

Mwaka 2010, Arsenal ilifungwa na Barca mabao 4-1 katika mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya awali kutoka sare ya mabao 2-2.

Lakini Barcelona, ambayo haijaruhusu kufungwa katika mechi tatu zilizopita, itatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kukabiliana na Arsenal.
by Lucy Turner
from Barcelona
Guardiola on the offensive against ArsenalJosep Guardiola promised that Barcelona will give their all against Arsenal
Nahodha Carles Puyol bado anasumbuliwa na goti na Gerard Pique ana kadi nyekundu.

Kocha Pep Guardiola, anayesumbuliwa na maumivu ya mgongo, atatakiwa kupanga mabeki ambao hawafahamiki sana.



No comments:

Post a Comment