Watani wa jadi nchini Simba na Yanga wanajiandaa na pambano la kukata na shoka litakalofanyika kesho ambalo linatarajia kumaliza ngebe za watani hao ambao wamekuwa akitambiana kwa muda mrefu sasa. Huku maandalizi hayo yakiendelea klabu ya Simba imemtema mchezaji aliewahi kuichezea klabu ya Yanga pia Mohamed Banka kwa utovu wa nidhamu kwa kutoroka kambini baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, huku baadhi ya wachezaji wa klabu ya Simba kama Emanuel Okwi na Jerry Santo wakiwataka mashabiki watulie kwani ushindi upo ili kulipa kisasi cha raundi ya kwanza ambapo Simba walifungwa goli 1 na Yanga.
Kikosi cha Simba 2011.
Huku hayo yakiendelea klabu ya Yanga imemtema mchezaji wake wa kimataifa toka Ghana Ernest Boakye kutokana na utovu wa nidhamu kwa kugomea mazoezi na kudai kocha wao mganda Sam Timbe anwapa mazoezi magumu
Kikosi cha yanga 2011
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam katika uwanja wa UHURU.
No comments:
Post a Comment