WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Wednesday, March 16, 2011

MAN UTD, INTER MILAN ZAFUZU ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE

  Manchester United na Inter Milan jana usiku zilikata tiketi za kucheza hatua ya robo fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya baada ya kushinda michezo ya marudiano. Manchester United ilishinda goli 2 - 1 dhidi ya Marseile ya Ufaransa katika dimba la Old Trafford baada ya kwenda sare katika mchezo wa katika mchezo wa awali huko Ufaransa, magoli yote ya Manchester United yaliwekwa kimiani na Chicharito katika vipindi vyote viwili moja ya vivutio vya mchezo ikiwa kuumia kwa mabeki O'shea na Raphael katika mazingira yanayofanana.
    Inter Milan nao walishinda kwa mbinde kwa kuwalaza Bayern Munich kwa bao 3 - 2 katika dimba la Allianz Arena mjini Munich huku wakionekana kuzidiwa kiufundi ila bahati ilikuwa yao baada ya Samuel Etoo' kutangulia kufunga goli la ufunguzi katika kipindi cha kwanza dakika ya 4 lakini Bayern walisawazisha kupitia Mario Gomez na Thomas Mueller huku Arjen Robben akionekana kuwa mwiba mkali dhidi ya Inter, Inter waliizinduka kipindi chapili na kupachika goli la pili kupitia Wesley Snijder na baadae katika dakika ya 87 Goran Pandev alipachika goli lililoipa ushindi Inter kwa faida ya kufunga goli nyingi ugenini. michezo mingine itaendelea leo ambapo Chelsea watawaalika F.C Compenhaggen na Real Madrid watukuwa wenyeji wa Olympic Lyon mechi yenye mvutano mkubwa wa kihistoria, mechi zote zitachezwa saa 4:45 kwa saa za Afrika mashariki.

Picha za Inter na Manchester United hapo jana
 Tuesday
Javier Hernandez akishangilia goli la kwanza dhidi ya Marseile
 Tuesday
Javier Hernandez akishangilia
 Tuesday
Lucho Gonzalez na Paul Scholes katika hekaheka
 Tuesday
Luis Nani akidhibitiwa na mabeki wa Marseile
 Tuesday
Rooney akiwa katika hekaheka
 Tuesday
Alex Ferguson akiingia uwanjani
 Tuesday
Raphael da Silva akikabana na Andrew Ayew wa Marseile
 Tuesday
Chicharito akipachika goli la pili
 Tuesday
Wachezaji wa Marseile wakishangilia goli la kujifunga la Brown
 Tuesday
Samuel Etoo akipachika golia kwanza dhidi ya Bayern
 Tuesday
Mario Gomez akisawazisha goli dhidi ya Inter Milan
 Tuesday
Thomas Mueler na Mario Gomez wakishangilia goli
 Tuesday
Thomas Mueller akipachika goli la pili dhidi ya Inter Milan
 Tuesday
Kocha wa Bayern Munich Louis Van Gaal akishangilia goli
 Tuesday
Thomas Mueller akishangilia goli la pili dhidi ya Inter Milan
 Tuesday
Wesley Snijder akipiga faulo dhidi ya Bayern Munich
 Tuesday
Wesley Snijder akishangilia goli la pili alilofunga dhidi ya Bayern
 Tuesday
Goran Pandev wa Inter Milan akipachika goli la tatu dhidi ya Bayern Munich
 Tuesday
Kocha wa Inter Milan Leonardo akishangilia pamoja na wachezaji wake
 Tuesday
Beki wa Bayern Holger Badstuber akiwa haamini baada ya mchezo kumalizika


No comments:

Post a Comment