WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Thursday, November 3, 2011

2.2 BILIONI ZATUMIKA KUWASOMESHA WATATU TCRA NJE KWA MWAKA:MALIPO YA ZIADA 36MILIONI. TUTAFIKA?

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC) imegundua ufisadi wa kutisha uliokuwa unafanyika ndani ya Bodi ya TCRA iliyo chini ya Jaji Buxton Chipeta. Akizungumzia swala hilo bwana Deo Filikijombe ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge inayoshughulikia matumizi ya mashirika ya umma alisema pesa nyingi zilizoorodhesha katika taarifa ya matumizi ya bodi hiyo zimetumika kifisadi na pakiwa na mazingira ya wazi ya ubadhilifu wa pesa za umma.
Miongoni mwa matumizi hayo ni shilingi
bilioni 2.2 zilizotumika kusomesha watendaji watatu wa mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka 2009/10 na kwa ujumla mpaka mwaka huu bodi hiyo imetumia bilioni 4.1 kwa ajili ya kugharamia mafunzo kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo, swali la kujiuliza ni kwamba hawa waliogharimiwa mabilioni haya mbona mchango wao katika jamii? Wanafunzi wengi wa Vyuo vikuu wanakosa mikopo ambayo ingewawezesha kusoma jambo ambalo lingechangia kuongeza idadi ya wasomi nchini. Watanzania wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku, wapi zinapatikana pesa hizi za kuwalipia vigogo hawa? Zinatoka mfuko gani?
Matumizi mengine ya kifisadi yaliyopingwa na (POAC) ni pamoja na shilingi milioni 36 zinazodaiwa kutumika kuwalipa wafanyakazi saba wa ofisi za uhasibu za mamlaka hiyo wanaodaiwa kufanya kazi muda wa ziada, dola
2,000 sawa na shilingi 3.4 milioni ambazo hutumika ajili ya mawasiliano ya bodi hiyo kwa mwezi, pia wafanyakazi wa bodi hiyo walipatiwa simu za mkononi kila mmoja zenye thamani ya dola 600 kila moja sawa na shilingi milioni 1 na wajumbe wa bodi hiyo wamekuwa wakilipwa dola 350 kila mwezi sawa na shilingi 600,000.
Filikijombe amesema kamati hiyo inashangwazwa kwanini wafanyakazi hao walipwe kwa dola baada ya shilingi? Huku akiainisha kuwa malipo ya dola 350 kwa mwezi sio sahihi kwao sababu wao sio watendaji wa kila siku wa mamlaka hiyo pamoja na dola 2,000 za mawasiliano.
Matumizi mengine ya mamlaka hiyo ni sambamba na kutumika kwa shilingi 45 bilioni katika ujenzi wa jengo hilo tofauti na ile iliyotajwa mwanzo ya shilingi 27 bilioni, pia pesa nyingine ni shilingi 600 milioni zilizotumika kwa manunuzi ya samani mbalimbali katika ofisi hizo.
Akijibu tuhuma hizo mwanasheria wa TCRA Elizabeth Nzagi amesema sio kweli kuwa mamlaka hiyo imekiuka taratibu za matumizi ya fedha za umma, akitetea kuwa mafunzo ya mambo ya mawasiliano ni gharama kubwa ndio maana wametumia 4.1 bilioni katika kipindi hicho na kwamba sio kweli kati ya hizo bilioni 2.2 zilitumika kusomesha wafanyakazi watatu kwa mwaka akidai kuna makosa ya kihasibu, swali linakuja tena hapa, inamaana hawakuisoma hiyo taarifa kabla ya kuiwakilisha? Au waliandikiwa?. Kuhusu milioni 36 zilizotumika kuwalipa wafanyakazi saba waliofanya kazi muda wa ziada amedai ni kutokana na uchache wa wafanyakazi, swali la kujiuliza wasomi wangapi wanahaha mitaani kutafuta ajira? Au hawana sifa?
Huu ni mtihani na hebu wenzangu mnaowaza mbali tazameni sinema hii mara mbili kisha mtoe tathimini, na cha kishangaza hakuna hatua zitakazochukuliwa zaidi ya kuunda tume.
Nchi imeoza, inanuka Rushwa na Ufisadi

No comments:

Post a Comment