WELCOME

MAY GOD BLESS YOU ALL FOR VISITING THIS SITE, A HOPE YOU WILL ENJOY EVERYTHING YOU GET HERE AND IF THERE Z ANYTHING BORING OR SHALLOW LEAVE COMMENTS PLEASE.
BE BLESSED

MY DIARY

My photo
Dar es Salaam, Tanzania, Tanzania
FRIEND TO EVERYONE AND I BELIEVE EVERYTHING IS POSSIBLE

RONNIE DOCOMENTARY

Popular Posts

Saturday, November 5, 2011

RAIS KIKWETE AMTEMBELEA VENGU HOSPITALI

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete jana alimtembelea msanii maarufu wa kundi la Origino Komedi anaejulikana kwa jina la kisanii Vengu katika Hospital ya Taifa Muhimbili. Akizungumza kwa kifupi moja ya ndugu wa familia amesema anashukuru sana kwa jinsi baadhi ya viongozi wa Serikali wanavyofika hospitalini hapo kumjulia hali mgonjwa na akasema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri tofauti na awali alipofikishwa hospitalini hapo.
Vengu 28, amelazwa hospitalini hapo kwa wiki kadhaa sasa ambapo hali yake imekuwa ya kusuasua huku tatizo linalomsumbua likiwa halijawekwa wazi na wanafamilia. Msanii huyo ambae alijipatia umaarufu katika kundi hilo kwa kuigiza kama baadhi ya wanasiasa maarufu nchini akiwamo Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa jimbo la Vunjo Mh Augustine Lyatonga Mrema amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miezi mitatu sasa ambapo mapema mwezi wa nane alilazwa hospitalini na kuruhusiwa na baadae kurejeshwa tena hospitalini hapo. Tumuunge Rais mkono kwa kwenda kumuona msanii huyu na kumuombea

No comments:

Post a Comment