Timu kongwe ya Manchester United imetupwa nje ya michuano ya Carling cup na Timu ya dataja la pili ya Crystal Palace kwa magoli 2 - 1.
Mchezo huo yliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford umeshuhudia Crystal Palace wakipata magoli yao kupitia kwa Darren Ambrosse 65' na jingine katika dakika za nyongeza kupitia kwa Glenn Murray 98' ambapo Manchester United walipata goli kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Federico Macheda 69'.
Haya yamekuwa matokeo mabaya zaidi kwa Manchester a,bao wanaonekana kusuasua baada ya sare mbili katikati na mwishoni mwa wiki dhidi ya Benfica katika Klabu Bingwa Ulaya na Newcastle United katika ligi ya Uingereza.
WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA
23 minutes ago
No comments:
Post a Comment