Moto mkubwa umezuka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya ubungo ambayo imepelekea baadhi ya Transformer kuendelea kuungua.
Moti huo ambao chanzo chake hakijafahamika unaendelea kuunguza mitambo hiyo huku pakiwa hakuna jitihada zozote za kuzima moto huo.
Uzembe uliojionyesha dhahiri ni kukuosekana kwa maji kwa gari la zimamoto ambalo hupaki pembezoni mwa mitambo ya Songas.
Hali inaonekana kuwa mbaya zaidi na foleni ni kubwa jambo ambalo litakuwa gumu kwa gari za zimamoto zinazotoka mbali na eneo hili. Idadi kubwa ya wafanyabiashara ambao hupanga bidhaa zao maeneo haya wanakusanya vitu vyao ili kurejea majumbani huku transformer mbili zikiendelea kuteketea
Tega sikio zaidi nipo eneo la tukio
WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA
11 minutes ago
No comments:
Post a Comment