Polisi mkoani Arusha leo alfajiri katika muda wa saa kumi na moja wamevamia katika viwanja vya NMC na kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliouanza mkesha maalumu toka jana ili kushinikiza serikali kumwachia huru mbunge wao Mh. Godbless Lema ambae anashikiliwa na polisi kwa takribani wiki nzima sasa.
Habari zinaendelea kusema pia polisi hao ambao walikuwa wakitumia mabomu ya machozi, virungu na risasi ambazo bado hazijafahamika kama ni za moto au plastiki wanamshikilia Katibu mkuu wa Chama hicho Mh. Wilbroad Slaa kwa mahojiano zaidi juu ya mkesha huo.
Habari zaidi baadae
Shinda Sehemu ya Bilioni 1.5 ya Lucky Rush
6 minutes ago
No comments:
Post a Comment