Kinyang'anyiro cha Urais wa mwaka 2015 umeendelea kuwapa tumbo joto baadhi ya vigogo wa CCM huku kila mmoja akitumia kila njia kuhakikisha yeye ndie anapitishwa kama mgombea.
Fukuto kubwa linaonekana kwa vigogo watatu wenye nguvu ndani ya Chama hicho ambao wamekuwa wakitumia kila njia kuhakikisha majina yao yanang'ara.
Baadhi ya vigogo hao wamekuwa wakihusishwa na mpasuko mkubwa unaoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi, ambapo baadhi wamekuwa wakiunga mkono wale wanaojihusisha na ufisadi wang'olewe ndani ya Chama, wengine wakipinga hilo na baadhi wakionekana kutounga mkono upande wowote.
Wengine wameenda mbali zaidi na kudai kuwa Rais ajae lazima atoke dini fulani kutokana na mlolongo wa wale waliopita kufuata mapokezano ya dini ambapo imekuwa wanaanza Wakristo na kufuatia Waislam jambo ambalo limewapa nguvu baadhi ya vigogo hao ambao ni wakristo kudhani kuwa sasa ni zamu yao. Huku hayo yakiendelea vyama vya upinzani vimeendelea kujipanga kuhakikisha nao wanachukua madaraka na jambo kubwa ambalo wanafanya sasa ni kuhakikisha wanajijengea sifa nzuri kwa wapiga kura.
WAZIRI MCHENGERWA AWAFUNDA MA RC WAPYA
10 minutes ago
No comments:
Post a Comment